GPSA YAOKOA ZAIDI YA SH. BILIONI MOJA ZA SERIKALI KUPITIA MPANGO WA MANUNUZI YA PAMOJA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:44 PM
Na Mwandishi Wetu
Serikali
kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), imeokoa sh
bilioni 1.3 baada ya wakala hiyo kununua kwa pamoja magari 392 katika
mpango wa serikali wa manunuzi ya pamoja.
Kaimu
Mtendaji Mkuu wa GPSA, Jacob Kibona, amesema jana kuwa fedha hizo
zimeokolewa na serikali baada ya kununua magari 392 kwa pamoja kwa Sh.
bilioni 56.1 badala ya sh. 58.1 kama kila taasisi ingenunua magari yake.
“Kwa
kweli huu mpango wa manunuzi ya pamoja ni mpango mzuri sana ambao
unaiwezesha serikali kuokoa fedha nyingi hivyo unapaswa kupewa
kipaumbele ili kuthibiti upotevu wa fedha kupitia,” Alisema Kibona.
Alisema
fedha zilizookolewa zitaiwezesha serikali kufanya shughuli nyingine za
maendeleo ya umma kama kuboresha miundombinu ya barabara, huduma za afya
na elimu.
Kibona
alisema katika kipindi cha Julai hadi Oktoba mwaka huu, GPSA
imezikabidhi taasisi za serikali magari ya aina mbalimbali yapatayo
136.
Alisema
katika kuhakisha kwamba wanapunguza gharama katika manunuzi, wamekuwa
wakinunua bidhaa kutoka kwa wazalishaji moja kwa moja ila
inaposhindikana kutokana na sera za kampuni kubwa kuwa na mawakala wa
usambazaji wamekuwa wakinunua kwa mawakala hao kwa makubaliano maalum ya
kupunguziwa bei.
Kibona
alisema kuwa kazi nyingine muhimu ya taasisi yake ni kugomboa mizigo
kupitia bandarini , viwanja vya ndege na mipakani kwa niaba ya serikali
ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita waligomboa mizigo yenye thamani ya
Sh. bilioni 62.7.
Alisema
mizigo hiyo ilikuwa ni pamoja na vifaa vya mkongo wa taifa wa
mawasiliano, vifaa vya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wizara
yaMaliasili na utalii.
Aliongeza
kuwa kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu pia
walikomboa vifaa mbalimbali vya serikali zikiwamo ndege mbili aina
yaBombadier, zilizonunuliwa na serikali kutoka Canada, vyote vikiwa na
thamani ya Sh. bilioni 100.97.
Kibona
alisema GPSA ina huduma za kuhifadhi vifaa kwa ajili ya taasisi za
serikali, kwa kuwa wao wana maghala makubwa katika mikoa karibu yote .
“Hata
mkoani Kagera baada ya maafa ya tetemeko la ardhi, maghala yetu
yanayotumika kuhifadhi vifaa mbalimbali viliyotolewa kama misaada,”
Alisema
pi wana jukumu la kutoa huduma ya mafuta kwa magari yaserikali na
kwamba kwamba hadi sasa wamefanikiwa kusimika mfumo wa usimamizi wa
mafuta kwa matumizi ya ya serikali na kwamba mfumo huo unaendelea
kupanuliwa ili uzifikie taasisi nyingi za umma.
Kibona
alizishauri taasisi za umma kuzingatia sheria za manunuzi kwa lengo la
kutoa huduma bora na kwa kuhakikisha kuwa vifaa na huduma zinazopatikana
zinazingatia thamani halisi ya fedha zinazotumika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: