WAZIRI UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA YA KIKAZI IFAKARA, MOROGORO
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 6:49 AM
Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi
katika hospitali ya Rufaa ya St. Francis pamoja na wajawazito
wanaosubiri kujifungua na ambao wapo chini ya uangalizi wa madaktari.
Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefanya ziara ya
siku 1 mjini Ifakara kufuatilia utendaji wa shughuli mbalimbali za Afya
Wilayani Kilombero, Morogoro.
Katika
ziara hiyo,
Ummy ambae alieambatana na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Florence
Tonguely-Mattli alifungua kozi ya miezi mitatu ya kutoa huduma
ya dharura ya afya kwa kina mama wajawazito hususani katika eneo la
upasuaji na utoaji wa dawa za usingizi.
Mafunzo hayo
yanayoendeshwa na Taasisi ya Mafunzo ya Kimataifa ya Afya (TTCIH) chini
ya Mradi wa "Upatikanaji wa Uzazi Salama Tanzania" yanawahusisha
Washiriki 70 kutoka mikoa ya Morogoro, Njombe na Mbeya.
Mhe Ummy pia alikagua
shughuli mbalimbali za taasisi za afya ikiwemo kutembelea Taasisi ya
Utafiti ya Ifakara (Ifakara Health Institute), Hospitali Teule ya Rufaa
ya St. Francis, Chuo cha Uunguzi cha Edgar Malanta na Chuo Kikuu cha
Tiba cha St. Francis.
Ummy Mwalimu
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Kimataifa ya Afya
(TTCIH) Prof. Pemba, Balozi wa Uswisi nchini Florence
Tonguely-Mattli.
Picha ya pamoja.
Ummy Mwalimu akizungumza
na washiriki wakati wa kufungua mafunzo ya miezi mitatu ya kutoa huduma
ya dharura ya afya kwa kinamama wajawazito katika taasisi ya
TTCIF, Ifakara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: