WAZIRI KITWANGA ATOA MSAADA WA BAISKELI 120 KWA MAKATIBU WA MATAWI CCM JIMBONI KWAKE MISUNGWI

11
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Jimbo lake mara baada ya Mbunge huyo kutoa msaada wa Baiskeli 120 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22 kwa ajili kutumika jimboni humo katika shughuli mbalimbali za chama. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Misungwi ambapo makatibu wote wa matawi walikabidhiwa baiskeli hizo.
12
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu akizungumza na Wanachama wa CCM wa Jimbo la Misungwi mara baada ya Katibu huyo kukabidhiwa Baiskeli 120 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, Charles Kitwanga (wanne kulia mstari wa mbele). Baiskeli hizo walikabidhiwa makatibu wote wa matawi wa CCM jimboni humo ili ziweze kurahisisha usafiri katika kazi mbalimbali za chama jimboni humo.
9
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akimkabidhi Baiskeli 120 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu kwa ajili ya kuwakabidhi makatibu wa matawi wa CCM Jimbo la Misungwi ili ziweze kutumika kwa ajili ya shughuli za chama jimboni humo. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi ya Wilaya ya Chama hicho, mjini Misungwi.
10 
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu (kushoto) akiwakabidhi Baiskeli baadhi ya makatibu wa matawi wa CCM wa Jimbo la Misungwi, mara baada ya Katibu huyo kukabidhiwa Baiskeli 120 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 22, na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo, Charles Kitwanga (kulia).  Baiskeli hizo ambazo zitatumika katika shughuli za kichama jimboni humo zilikabidhiwa katika ofisi za chama hicho, mjini Misungwi leo.
Picha zote na Felix Mwagara.

0 comments: