RAIS DKT. MAGUFULI NA RAILA ODINGA WASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA PILI YA PASAKA CHATO MKOANI GEITA.
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:22 AM
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga wakisali katika kanisa la
Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli amesali
ibada ya jumapili ya pili ya Pasaka tangu kuchaguliwa kuwa Rais.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga pamoja na Mke wa Raila
Bi. Ida Odinga wakifatilia kwa makini mahubiri ya Paroko Padre Henry
Mulinganisa katika ibada ya pili ya pasaka Chato Mkoani Geita.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Bi.
Ida Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na Rais
Dkt. John Magufuli wakifatilia kwa makini mahubiri yaliyokuwa yakitolewa
katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga, Mke wa Raila Bi. Ida
Odinga pamoja na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakishukuru mara baada
ya ibada.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Sakramenti takatifu kutoka kwa Paroko
wa Parokia ya Bikira Maria Chato Padre Henry Mulinganisa .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: