MAKAMU WA RAIS SAMIA AFUNGUA KONGAMANO LA 21 KWA WATAFITI WA UCHUMI WA VIWANDA

MOR1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti inayohusiana na maendeleo ya Ustawi Nchini (REPOA) Professa Yadon M Kohi, kabla ya kufungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda iliyoanza April 06, 2016 katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari  Beach jijini Dar es salaam.
MOR3
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akifungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti inayohusiana na maendeleo ya Ustawi Nchini (REPOA) Warsha hiyo imefunguliwa  leo April 06,2016 katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari  Beach jijini Dar es salaam.
MOR4
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki, Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda baada ya kufungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa washiriki hao inayojadili kuhusu uendelezaji wa Utafiti wa Uchumi wa Viwanda Nchini. Warsha hiyo imefunguliwa, April 06,2016 katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari  Beach jijini Dar es salaam.
MOR5
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti inayohusiana na maendeleo ya Ustawi Nchini (REPOA) Professa Yadon M Kohi, baada ya kufungua Warsha ya 21 ya Mwaka kwa Wasomi na Watafiti wa mambo ya maendeleo ya Uchumi wa Viwanda April 06,2016 katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es salaam. (Picha na OMR)

0 comments: