Inaelekea kuwa, iwapo mchakato wa sasa wa mashindano ya ndani ya chama cha Republican utaendelea katika majimbo yaaliyosalia Marekani, Trump ataendelea kuongoza na kuna uwezekano mkubwa akapata nafasi kubwa ya kuteuliwa katika kongamano la kitaifa cha Warepublican kuwa mgombea atakayechuana na mgombea wa Wademocrat. Ni kwa sababu hii ndio wakuu wa chama cha Republican kidhahiri wakaonekana kuingiwa na wasiwasi mkubwa kutokana na uwezokano wa mtu mwenye misimamo mikali na ya kufurutu ada kama Trump kuteuliwa na wafuasi wa chama hicho kuwania urais. Vinara wa chama cha Republicana wana hofu kuwa iwapo mtu kama Trump atachaguliwa kura rais basi Marekani itakumbwa na matatizo makubwa na pia kuchafulia jina chama hicho kikingowe.
Kwa maelezo hayo, kutokana na kuwa Trump anaongoza kwa idadi kubwa ya kura za ndani ya chama ikilinganishwa na wapinzani wake, kuna uwezekanao wa baadhi vya vigogo ndani ya chama wakatumia mbinu kadhaa kumuondoa katika mchuano wa urais.
Trump aliwahi kutishia kuwa, iwapo vinara wa chama cha Republican watamuondoa pamoja na kuwa na kura nyingi, basi atagombea urais wa Marekani kama mgombea huru.
Lakini sasa kwa mara ya kwanza, Trump ametoa vitisho kwa Warepublican kuwa iwapo watamnyima haki ya kuwania urais basi mamilioni ya wafuasi wake wataandamana na kuibua ghasia katika mitaa ya Marekani.
Kwa msingi huo tunaweza kusema kuwa, mchuano wa ndani ya vyama nchini Marekani umekumbwa na masuala ambayo hayajawahi kushuhudiwa siku za nyuma. Moja ya mambo mapya yaliyoshuhudiwa ni mapigano na makabiliano baina ya wafuasi wa Trump na wapinzani wake katika mikutano ya kampeni ya mgombea huyo. Trump anawatuhumu wagombea wa chama cha Democrat kuwa wanatuma magenge ya wapizani kuibua ghasia katika mikutano yake ya kampeni. Kwa kuwatuhumu wenzake, Trump anataka kuwashawishi Wamarekani kuwa ana umashuhuri zaidi kuliko wagombea wengine, hasa Hillary Clinton.
Trump ametoa mamtamshi ya utata mara kadhaa dhidi ya wahajiri wenye asili ya Mexico na Waislamu Marekani. Tunaweza kusema kuwa Trump anatumia matatizo yaliyopo Marekani kama vile ugaidi ili kupata kura za Wamarekani kwa kutoa ahadi kama vile kuboresha uchumi na hali ya kijamii ya Wamarekani
0 comments: