TCRA WAPELEKA BIL. 40.6 MFUKO WA SERIKALI (HAZINA)

Dk.Ally Simba
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema mpaka sasa mamlaka imepeleka fedha kwenye mfuko wa serikali (hazina) kiasi cha Sh. 40,656,865,447.03 ambazo nimakusanyo ya kuanzia Oktoba, 2013 hadi Agosti, 2015.
Hayo yamesemwa Dar es salaam, wakati wa mkutano wa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mamlaka ya mawasiliano, Mkurugezi mkuu wa Mawasiliano Tanzania, Dk.Ally Simba.
Pia alisema kumesaidia kuweza kudhibiti mawasiliano ya ulaghai na hivyo kuweza kudhibiti vitendo viovu vinavyofanyika kupitia njia hiyo na kuimarisha usalama nchini.
“Kifungu cha 6(1) kinaelezea kanuni za TTMS zinaitaka mamlaka ya mawasiliano kuwasilisha asilimia 28 ya mapato yatokanayo na mtambo wa kuhakiki mawasiliano ya simu kutoka nje ya nchi katika mfuko mkuu wa serikali,” alisema Simba.
Dk.Simba alisema kuwa mfumo wa kusimamia mawasiliano TTMS umesaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa sheria na kanuni zilizopo katika kudhibiti sekta ya mawasiliano.
Aidha alisema mamlaka imefanikiwa kufunga mitambo kwa watoa huduma katika maeneo 13, ikiwepo Dar es Salaam na Zanzibar, pia TCRA itaendelea kushirikina na jeshi la polisi ili kukabiliana na mawasiliano ya siyo ya halali.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ambaye ni mbunge wa Makete, Prof. Norman Sigalla alitumia fursa hiyo kuzitaka mamlaka zote zinazo shirikiana na TCRA kutoa anuani za makazi ili zikamilike mapema, katika kuhakikisha wana simamia shughuli hizo na kuahkikisha wanamalizika kwa wakati kwani siku hazirudi nyuma.
Na Mary Mtaki.

0 comments: