SIMBA IMEKUWA KLABU YA KWANZA KATI YA AZAM FC NA YANGA, KUPATA USHINDI DHIDI YA COASTIL TANGA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:16 PM
Baada ya uwanja wa Mkwakwani kutajwa kuwa mgumu msimu huu kupata matokeo kwa Yanga na Azam FC, March 19 ilikuwa ni zamu ya wekundu wa Msimbazi Simba kupambana na Coastal Union ambapo kwa Yanga na Azam FC zote ziliambulia kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Coastal Union.
Simba walikuwa wanatizamiwa kupata wakati mgumu kama walikokuwa wameupata Yanga na Azam FC, kitu ambacho kiliwafanya waanze mchezo kwa umakini mkubwa, Coastal walionesha jitihada kiasi, lakini juhudi za Simba zilizaa matunda dakika ya 39 baada ya Danny Lyanga kupachika goli la uongozi kwa Simba.
Kipindi cha kilimalizika kwa Simba
kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0, goli ambalo lilikuwa chachu
ya wao kuendelea kufanya vizuri katika mchezo huo, kipindi cha pili
dakika ya 51 Hamis Kiiza alitumia vizuri krosi ya Emily Nimubona na kupiga kichwa kilichozaa goli la pili.
Hadi dakika 90 zinamalizika Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 na kupata point tatu, kwa matokeo hayo Simba anaendelea kuongoza Ligi kwa jumla ya point 57 akiwa kacheza michezo 24, lakini kawazidi Yanga na Azam FC point saba na michezo mitatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: