Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa wizara hiyo imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na katika kipindi cha mwezi Februari mwaka huu zimekusanywa zaidi ya Sh. trilioni 1 tofauti na mwanzo ambapo zilikuwa zkikusanywa Sh.bil 850. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mpoki Ulusubisya.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam jinsi Mamlaka hiyo ilivyofanikiwa kukusanya mapato kutoka trilioni 1.2 kwa mwezi Disemba mpaka trilioni 1 na bilioni 79 kwa mwezi Januari na kwa mwezi Februari wanatarajia kukusanya trilioni 1.013 na tayari wamefikia nusu ya malengo waliyojiwekea.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknologia na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Maimuna Tarishi amesema Wizara yake itazitumia fedha walizopewa mwezi huu kulingana na malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Diploma na wanafunzi wa chuo kikuu. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) Alphayo Kidata

Katibu Mkuu Wizara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee akifafanua namna Wizara yake ilivyojipanga kuzitumia fedha walizopata mwezi huu ambapo amesema zitatumika kulingana na malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za mradi wa ujenzi wa Chuo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili eneo la Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

 Waandishi habari wakikusanaya taarifa

0 comments: