Watu 62 wamefariki dunia mapema leo baada ya ndege ya abiria ya
Shirika la Fly Dubai kuanguka wakati ikijaribu kutua katika mji wa
Rostov-on-Don kusini mwa Russia karibu na mpaya wa nchi hiyo na Ukraine.
Ripoti zinasema kuwa ndege hiyo iliyotengenezwa Marekani aina ya
Boeing738-800 ilianguka ikijaribu kutoa ikiwa imetoka Dubai nchini
Imarati.
Msemaji wa Wizara ya Maafa nchini Russia Marina Kostioukova
amethibitisha kutokea ajali hiyo lakini hakutoa maelezo zaidi. Abiria
wote 55 na wahudumu 7 katika ndege hiyo wamepoteza maisha.
Shirika la Habari la RT limeripoti kuwa, uchunguzi wa awali umebaini
kuwa ndege hiyo imeanguka kutokana na hali mbaya ya hewa katika uwanja
huo wa ndege.Aghalabu ya abiria katika ndege hiyo ni raia wa Russia.
Duru zinaarifu kuwa ndege hiyo ilijaribu kutua mara ya kwanza na
kushindwa na kuanguka ilipojaribu kutua kwa mara ya pili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: