Na Dotto Mwaibale
MUTFI WA TANZANIA AMUOMBEA DUA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 8:32 AM
Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubery akiwa nyumbani kwake.
Mufti
wa Tanzania, Abubakar Zubery (wa pili kushoto), akimuombea dua Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), Dar es Salaam leo
asubuhi. Kutoka kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi
Mussa Salum, Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid na Msaidizi
wa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Othman Mkambaku.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum (kulia), akizungumza na wanahabari kabla ya kufanyika dua hiyo. Kushoto ni Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid.
Mufti Zubery, akifanya mazungumzo na Makonda.
Dua ikiendelea nyumbani kwa mufti Mikocheni.
Wapiga picha kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Makonda akiagana na Sheikh Abubakar Khalid na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.
Na Dotto Mwaibale
Na Dotto Mwaibale
MUFTI
wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubery amemuombea dua, Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam pamoja na Rais Dk. John Magufuli ili waweze kulitumikia vema
taifa na kuliletea maendeleo.
Zubery
alimfanyia dua hiyo Makonda Dar es Salaam leo asubuhi alipofika
nyumbani kwake kujitambulisha na kumjulia hali pamoja na kumueleza mambo
kadhaa ya maendeleo yaliyofanyika.
"Tunakuomba
mola wetu kuwapa moyo wa imani na uzalendo na kuwaepusha na mabaya yote
Mkuu wetu wa Mkoa Paul Makonda, Rais wetu Magufuli pamoja na viongozi
wote ili waliongoze taifa letu kwa amani" alisema Mufti Zubery" wakati
akiomba dua hiyo.
Makonda
akizungumza na Mufti Zubery nyumbani kwake Mikocheni alimwambia kuwa
kuna mambo kadhaa ameyafanya kwa kushirikiana na watendaji wenzake kwa
kukutana na waendesha boda boda ili kuwawezesha kupata mkopo
utakaowasaidia kupata vitendelea kazi zao kama kupata kofia ngumu mbili
za kuvaa dereva na abiria wake ili kuwasaidia katika shughuli zao za
kusafirisha abiria.
Makonda
alitaja mambo mengine kuwa ni suala nzima la kupambana na uhalifu ambao
bado unaonesha kupamba moto hasa ujambazi wa kutumia silaha za moto.
Alitaja
mambo mengine kuwa ni mkutano alioufanya hivi karibuni wa kukutana na
wenyeviti wa mitaa na maofisa watendaji ili kuzungumzia suala la
utunzaji wa mazingira na mambo mengine ambapo alisema ameandaa mpango wa
kumzawadia mwenyekiti atakayefanya vizuri kwenye mtaa wake.
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum alisema jambo
alilofanya Makonda la kumtembea Mufti ni jambo zuri na kuwa kumuona
mufti ni sawa kama amewaona waislam wote nchini.
Alisema
wanamuombea Makonda mungu amzidishie wepesi katika kazi zake kwani ni
viongozi wachache wanaopata madaraka ambao uwakumbuka viongozi wa dini
kama alivyofanya Makonda.
Katika
hatua nyingine Makonda alifanya ukaguzi wa barabara kadhaa za Manispaa
ya Kinondoni ambazo hivi karibuni aliagiza zifanyiwe marekebisho ikiwa
ni pamoja na kuchimba mifereji baada ya kuharibika kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: