HALI HALISI YA ZANZIBAR USIKU HUU


Hali ya amani na utulivu visiwani
Zanzibar imeendelea kuwepo licha ya kuwepo na taarifa za kuwepo kwa vurungu
visiwani humo.
Katika baadhi ya maeneo visiwani
humo wananchi wameendelea na shughuli zao kama kawaida bila ya kuwepo vurungu
husasani katika maeneo ya biashara.

Wakizungumza kuhusu hali ya
usalama wananchi wasemema kuwa hali ya usalama imeimarishwa na hakuna vurungu kwani
jeshi la polisi limejipanga kulinda raia na mali zao.

Aidha mmoja wa wafanya biashara
katika eneo la darajani,Bw Rajabu Athuman Rajabu amesema kuwa,taarifa za kuwepo
vurungu visiwani humo zinapotosha na baadhi ya watu wasio takia mema Zanzibar

“kwa kweli amani ipo na
tunaendelea na biashara kama unavyoona watu wanapotosha na kuwafanya watu
waishi kwa wasi wasi,kwani ulizi upo wa kutosha”amesema Bw Rajabu.

Kwa upande wake Bi Amina Said
Salum mkazi Mazizini amesama kuwa Serikali Zanzibar inapaswa kutoa taarifa kwa
wananchi wake ili wajue hali halisi ya usalama viziwani humo.

Ameongeza kuwa serikali inajukumu
la kuangalia na kusikiliza maoni yanayotolewa na wananchi na kuyafanyia
kazi,”serikali itusikilize na kutoa taarifa kwa wakati ili kuondoa hofu kwa
watu”Bi Amina

Hata hivyo baadhi wa wananchi
visiwani humo wameoneka kuwa na shauku ya kupiga kura kwa na kutoa wito kwa
wananchi wenye sifa ya kupiga kura kujitokeza kwa wingi.

Aidha katika barabara ya Amani
majira ya saa mbili usiku taa za barabara hiyo zilionekana zikiwa zimewashwa na
wananchi kuendelea na maisha yao ya kaiwada.

Kwa upande wa vituo vya kupigia
kura vituo hivyo vimekamilisha utaratibu wa watu kuhakiki majina yao na
wafanyakazi wa tume wakiwa tayari kwa kazi ya kuongoza watu kupiga kura.

Wafanya kazi katika vituo hibyo
walionekana wakiwa wamepumzika baada ya kukamilisha kazi ya maandalizi,wamesema
kuwa vituo hivyo vitafunguliwa mapema ili kutoa nafasi kwa wananchi kupiga kura
kwa wakati.

0 comments: