DEREVA WA GARI LA MURO T382 CTN ALIA NA ASKARI WA MISIGIRI KWA TOCHI BARABABINI

 Dereva wa Gari T 382 CTN, alia na ukiritimba wa chini kwa chini na Tochi zisizo za msingi awapo Barabarabani, hayo yilitokea jana, baada ya Dereva huyo kutaka kuwaachia gari Askari hao  wakiwemo Abiri waliokua kwenye gari hilo baada ya kufika eneo la Misigiri kulazimishwa kulipa Fain (BAO) kwa lazima, Dereva huyo alishuka toka kwenye gari hilo na kwenda kuwasikiliza na kuomba aonyeshwe hilo tochi au picha iliyopigwa lakini hakuonyeshwa na Askari aliyekua akimwandikia bao hilo Kondakta wa gari hilo alipanda kwenye gari ili kujiridhisha na mwendo wa Dereva, alisalimi na kuwauliza abiria vipi mwendo wa Dereva? walipaza sauti zao kwa pamoja, mwendo wa Dereva ni mdogo mno na wakasema abiria hao, tumetoka Shinyanga saa 3.06 na tumefika eneo hili saa 6.57, lakini Askari huyo alishuka na kumpiga bao Kondakta huyo la nguvu lakini Konda huyo alitoa pesa kwa shingo upande na Risiti konda huyo hakupewa. Wapipofika Singida saa 8. 38,  Baadhi ya Abiria walimuuliza Askari mwenye namba F 9972 kutaka kufahamu taratibu, ndipo abiria walisema wanapo ulizwa abiria kua, abiria mnaonaje mwendo wa dereva wenu unaridhisha? iweje hawasikilizwi na kunafaidagani kuwauliza abiria na kuto wasikiliza? Askari huyo aliwaonyesha picha ya gari moja   iliyopigwa na kutumwa kwa njia ya WhatsAp, ni moja ya kupunguza ajali, Askari huyo alisema kwa Dereva huyo angekua anakwenda mwendo wa kasi asingekua hapa Singida , angekua amefika Dodoma,    ambapo baadhi ya abiria walimshukuru kwa kuwapa muongozo na askari huyo aliwatakia abiria safari njema abiria walimshukuru kwa ushirikiano na abiria waliomba askari wawe na moyo wa askari kama wewe kutolazimisha mambo.Gari hilo lilifika Dar es Salaam katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo mnamo mida ya Saa 7.30 usiku. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Askari akimwandikia kondakta huyo
 Konda akimpa pesa Askari huyo
 Askari akimuonyesha Kondakta huyo sehemu ya kuweka saini na Mmoja wa abiria katikati  akishuhudia konda akionyesha sehemu ya kusaini










 Askari akiwa ndani ya Gari katika Stendi ya Mabasi Singida akiwaanyesha Abiria waliokuwa kwenye basi hilo picha iliyopigwa kwa njia ya Mtandao.

0 comments: