WAZIRI MKUU ASISITIZA UMOJA KWA MAJESHI YA EAC

PG4A3786Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimina na wachezaji wa timu ya mpira wa Miguu ya Jeshi la Uganda katika kilele cha michuano  ya majeshi ya Nchi za Afrika ya Mashariki kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar August 29, 2014.. Katika mechi ya kufunga mashindahayo Uganda na Tanzania zilitoka sare ya 1-1. Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A3788Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimina na wachezaji wa timu ya mpira wa Miguu ya Jeshi la Uganda katika kilele cha michuano  ya majeshi ya Nchi za Afrika ya Mashariki kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar August 29, 2014.. Katika mechi ya kufunga mashindahayo Uganda na Tanzania zilitoka sare ya 1-1. Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………….
*Afunga michezo ya majeshi Afrika Mashariki
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hayana budi kuendeleza umoja na mshikamano ili kukuza udugu uliopo.
Ametoa kauli hiyo jana usiku (Ijumaa, Agosti 29, 2014) wakati akifunga mashindano ya Michezo ya Majeshi ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar.
Waziri Mkuu ambaye kabla ya kuhutubia umati ulioshiriki hafla hiyo, alikabidhi kombe kwa washindi wa soka, ambao ni timu ya Jeshi la Ulinzi la Kenya, alisema amefarijika kwa jinsi alivyoshuhudia mechi kati ya Tanzania na Uganda ikichezwa kwa staha bila vurugu zozote. Katika mechi hiyo, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na kuifanya Tanzania iibuke mshindi wa pili kwenye mchezo wa soka na Uganda kushika nafasi ya tatu.
“Michezo siyo chuki bali hujenga uelewano na mshikamano. Ni fursa ya kujenga mahusiano ya baadaye kwani hakuna ajuaye, huenda tukawa na jeshi moja la Jumuiya huko mbele,” alisema.
Alisema kutokana na ustadi ulioonyeshwa na wachezaji, wakuu wa majeshi waangalie uwezekano wa kutafuta mechi na jumuiya nyingine za Afrika Magharibi ama Afrika Kaskazini ili kujipima kwa kiwango kikubwa zaidi badala ya wao kwa wao. “Tujaribu kwenda nje ya Jumuiya yetu tukashindane nao kwa sababu nimeona uwezo mnao,” alisema.
Katika mashindano hayo yaliyoanza Agosti 19, 2014, Kenya iliibuka mshindi katika soka, Tanzania iliibuka mshindi kwenye Netiboli, Uganda kwenye mpira wa vikapu na Kenya ikashinda tena kwenye mpira wa mikono. Katika riadha, Tanzania ilishinda upande wa wanaume na Kenya ilishinda upande wa wanawake.
Michuano hiyo ambayo imefanyika kwa miaka minane mfululizo katika nchi wanachama, mwaka kesho, imepangwa kufanyika nchini Uganda.

0 comments: