Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
9:29 AM
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa
Japan, Hirotaka Ishihara baada ya kukutana naye Ofisini kwake jijini Dar
es salaam August 30, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amesema umefika wakati wa Japan kuhamia barani
Afrika na na kuwekeza kwa nguvu hasa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.Ametoa
kauli hiyo leo mchana (Jumamosi, Agosti 30, 2014) wakati alipokutana na
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Bw. Hirotaka Ishihara na
wafanyabiashara kutoka Japan kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya
Waziri Mkuu. Bw. Ishihara anaongoza ujumbe wa wafanyabiashara 70 kutoka
makampuni makubwa 14 ya Japan.Akizungumza
na Bw. Ishihara na baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo,
Waziri Mkuu alisema ni ukweli usiopingika kwamba Japan ni nchi yenye
uchumi imara na kwamba licha ya kuwepo kwa mikutano ya TICAD ambayo
hutoa fursa kwa Japan kushirikiana na nchi za kiafrika, bado kuna haja
ya wao kuelekeza macho yao Afrika kipekee.
“Mikutano
ya TICAD imekuwa ikifanyika kwa zaidi ya miaka 20 sasa lakini nchi za
Afrika na hasa Afrika Mashariki tumefumba macho… tumeshindwa kutumia kwa
kiasi kikubwa fursa zilizopo na kuchota utaalamu wa kiteknolojia kutoka
Japan,” alisema.
Waziri
Mkuu alisema Afrika Mashariki ni soko la uhakika kwa mtu yeyote
anayetaka kuwekeza barani Afrika. “Kama nchi wanachama wa Jumuiya siyo
soko la kutisha, lakini kutokana na mahali nchi zetu zilipo, tuna fursa
kubwa ya kufungua milango ya soko kwa nchi zote jirani zinazotuzunguka
na hiyo ni fursa kubwa kwa mwekezaji yoyote,” alisisitiza.
Kuhusu
uwekezaji, Waziri Mkuu alisema Japan inaweza kuwekeza kwenye viwanda
vya nguo na kusokota nyuzi, kuna fursa kwenye viwanda vya kusindika
samaki kwani kuna aina nyingi za samaki waliopo katika bahari ya Hindi.
Pia alisema amefarijika kusikia kwamba wameonana na wahusika kutoka
Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC).
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan ambaye ndiye
kiongozi wa msafara huo alimweleza Waziri Mkuu kuridhishwa kwake na
mahusiano yaliyopo baina ya nchi hizo mbili na kwamba katika kipindi cha
miaka miwili kumekuwa na ongezeko la ziara za viongozi baina ya nchi
hizi mbili.
“Nina
furaha kuzuru Tanzania kwa mara ya pili nikiongoza Kamati ya Pamoja ya
Umma na Sekta Binafsi ya Kukuza Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania…
tumevutiwa na kasi ya ukuaji uchumi wa Tanzania, ndiyo maana makampuni
ya Kijapani yameonyesha nia ya kuja kuwekeza nchini Tanzania,” alisema
Bw. Ishihara.
Bw. Ishihara na msafara wake wamemaliza ziara yao ya siku ya tatu hapa nchini na wanaondoka Tanzania kurejea Japan leo jioni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: