Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
2:06 PM
Mwili
wa abiria wa kike anayedaiwa kuwa na umri katika ya miaka 20-23
aliyefariki dunia kwenye ajali ya basi la KISBO iliyotokea katika kijiji
cha Kambi ya mkaa kata ya Issuna wilaya ya Ikungi.
Askari
wa usalama barabarani wilaya ya Ikungi, akikagua basi la kampuni ya
KISBO, T.534 CHX baada ya kupinduka katika eneo la kijiji cha Kambi ya
mkaa kata ya Issuna wilaya ya Ikungi na kusababisha vifo vya watu wawili
na kujeruhi wengine 52.
Na Nathaniel Limu, Singida
ABIRIA
wawili wamefariki dunia na wengine 52 kujeruhiwa vibaya baada ya basi
walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi la mbele kulia na kuacha barabara
na kisha kupinduka.
Basi
lililohusika na ajali hiyo ni T.534 CHX aina ya Scania mali ya kampuni
ya KISBO. Ajali hiyo inayodaiwa kuchangiwa na mwendo kasi ,imetokea
Agosti 21 mwaka huu saa 9.45 alasiri huko katika kijiji cha Kambi ya
mkaa kata ya Issuna,wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela alisema watu
hao waliopoteza maisha yao papo hapo,ni kijana wa kiume ambaye alikuwa
konda wa basi hilo anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 na 23 na
abiria wa kike anayekadiriwa kuwa na umri huo huo wa kati ya miaka
20-23.Wote wawili hadi sasa majina yao bado hayajulikana.
Alisema
basi hilo lililokuwa linatokea Dar-Es-Salaam likielekea Kahama mkoa wa
Singida, lilipofika eneo la tukio lilipasuka tairi la mbele kulia na
kuacha barabara na kisha kupinduka mara moja na kuserereka hatua zaidi
ya mia moja.
Basi
la kampuni ya KISBO T.534 CHX linavyoonekana baada ya kupasuka tairi la
mbele kulia na kuacha barabara na kisha kupinduka katika kijiji cha
Kambi ya mkaa kata ya Issuna wilaya ya Ikungi.
Alisema
basi hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Edward Paulo Temu (45) mkazi
wa jijini Dar-es-salaam ambaye inadaiwa siku hiyo ndiyo alikuwa
amekabidhiwa rasmi kuendesha basi hilo.
Kamwela
alisema katika ajali hiyo, abiria 52 kati yao 20 wamelazwa katika
hospital ya Misheni ya Puma na wengine 32 wamelazwa katika hospitali ya
mkona mjini hapa.
“Uchunguzi
wa awali unaonyesha wazi kuwa basi hilo lilikuwa katika mwendo kasi.
Naomba nitumie nafasi hii kutoa wito kwa wananchi kufika katika hospital
ya mkoa ,ili kuwatambua marehemu kwa ajili ya kufanya taratibu za
mazishi.
Kwa
upande mwengine natoa wito kwa madereva na watumiaji wengine wa
barabara,kufuata sheria kanuni na taratibu za usalama barabarani kama
njia moja wapo ya kupunguza ajali zinazochangia rai kupoteza maisha na
mali zao”,alisema Kamanda Kamwela.
Kwa
upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini
Singida,Dk.Deogratius Baluba alikiri kupokea miili ya watu wawili
waliofariki kwenye ajali ya basi la KISBO na majeruhi 32 ambao wengi
hali zao zinaendelea vizuri.
Katika
hatua nyingine,Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa ambaye
pia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone aliyefika kwenye eneo la
tukio akifuatana na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya
ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi,Alhaji Manju Msambya walionyesha
masikitiko yao kutokana na ajali hiyo na kutosita kukemea tabia ya
baadhi ya madereva wanaokwenda mwendo kasi unaosababisha ajali na vifo
vya abiria.
Askari
wa usalama barabarani wakuchukua maelezo kutoka kwa mmoja wa majeruhi
(amelazwa katika hospitali ya mkoa) wa basi la KISBO T.534 CHX aina ya
Scania lililopinduka baada ya kupasuka tairi katika eneo la kijiji cha
Kambi ya mkaa wilaya ya Ikungi.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: