KAMISHNA KOVA AUNGURUMA AMWAGA SIMU KWA ALBINO WOTE DAR ES SALAAM,AWAAHIDI NEEMA,ANASA PIA MABILIONI FEKI-CHEKI STORY NZIMA HAPA
|
Kamishna
wa polisi kand maalum ya dar es salaam Suleman kova akimkabidhi
mwenyekiti wa chama cha albino Dar es salaam simu kwa ajili ya albino
waishio jijini Dar es salaam
|
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya D’Salaam limewashauri albino wanaoishi Jijini
D’Salaam kuwa karibu sana na Jeshi hilo ili kurahisisha mawasiliano
kati yao na Wakuu wa vituo vya Polisi vilivyo karibu na makazi yao au
wanapofanyia usalama wao jijini D’Salaam.
Pamoja na kwamba haijawahi kutoa tukio lolote dhidi ya Albino
jijini D’Salaam kutokana na uhusiano uliopo lakini kwa sasa waongeze
mawasiliano na Jeshi la Polisi kutokana na taarifa za uhalifu dhidi ya
Albino katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Pia
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi D’Salaam SULEIMAN KOVA
ameongea na Albino hao ofisini kwake na kuwaambia kwamba Jeshi la Polisi
kwa ujumla linaendelea na jitihada kubwa sana kupambana na maadui wa
Albino ambao ni wahalifu na wengi wao wameishakamatwa na kufikishwa
mahakamani ambapo wengine wameishahukumiwa.
Albino wanatakiwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na Jeshi
la Polisi hata kama hakuna tishio la aina yoyote wanalolijua katika
maeneo yao ya makazi au wanapofanya shughuli zao za kikazi.
Katika
kufanikisha zoezi hilo la mawasiliano ya haraka na Jeshi la Polisi,
Kamishna wa Polisi Kanda Malum ya D’Salaam kwa kushirikiana na wadau
kampuni ya SAPNA ELECTRONIC ametoa simu 20 kwa Albino ambao wameudhuria
kikao ili iwe rahisi kwao kuwasiliana Jeshi la Polisi kwa namba
0787-668306 ambayo ipo katika chumba cha dharura katika Kikosi cha
999.
Kamishna Kova anaendelea kuongea na wadau mbali mbali
ili misaada zaidi ipatikane kwa walemavu wa ngozi ambao ni Albino ili
waweze kupata simu za mikononi, mafuta maalum ya kupaka ngozi zao na
msaada mwingine wowote ambao utafaa kwa Albino hao kupitia kwa namba
0715 – 009983 hii ni namba ya Kamishna mwenyewe ya oisi na namba
nyingine ya Msaidizi wake katika suala la kuwasaidia Albino ni
0756-710179 ambayo ni ya SP. MOSES NECKEMIAH FUNDI.
Aidha
zipo jitihada za makusudi zinazofanyika kati ya Polisi Kanda Maalum ya
Polisi D’Salaam na uongozi wa Mkoa na Kitaifa kwa manufaaa ya ulinzi na
Usalama wa Albino wote.
Hatua zingine za ziada za muda mfupi na mrefu ni uwepo wa
program ya mafunzo maalum kwa Albino wa Jijini D’Salaam ili wapate
mafunzo kupitia dhana ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kwa lengo la
kupata uelewa wwa kutosha ili nao pia washiriki na kujua namna ya kutoa
taarifa kwa lengo la kujikinga na maadui wao ambao wamegubikwa na tama
za kujipatia mali, madaraka n.k. kwa njia za ushirikina.
SABA WAKAMATWA KWA KUJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI WA NOTI BANDIA ZA DOLA ZA KIMAREKANI WAKAMATWA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata
kundi la watu saba wanaotengeneza noti bandia za Dolla ya Kimarekani
huko maeneo ya Sinza katika Hotel iitwayo Mombasa Kinondoni, jijini Dar
es Salaam. Watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 04/8/2014 wakiwa na
noti bandia zipatazo 10,640 za dola mia (100) ambazo ni sawa na DOLLA
1,064,000 (Dolla Millioni Moja na Sitini na Nne Elfu) sawa na shilingi
za kitanzania 1,702,400,000/= (TSH. Billioni Moja, Millioni Mia Saba na
Mbili na Laki Nne) katika nyumba namba 07 walimokuwa wamepanga.
|
Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam akionyeaha hela feki zilizokamatwa |
Polisi
walipata taarifa toka kwa wasamaria wema na kuweka mtego wa kuwakamata
ndipo askari walipofika eneo hilo waliwakamata watuhumiwa na noti za USD
bandi zikiwa zimefungwa mabunda themanini na kasiki ndogo ambayo
imefungwa kwa namba za siri.
Aidha watuhumiwa hao walikiri kujihusisha na utengenezaji wa noti bandia, watuhumiwa hao ni kama ifuatavyo;
1.AHMAD S/O MOHAMED Miaka 50, mfanyabiashara, mkazi wa Mombasa Kenya
2.ICHARD S/O MAGOTI Miaka 61, mfanyabiashara, mkazi wa Musoma mkoani Mara.
3.SIMONI S/O LUKIKO Miaka 58, mkazi wa Magomeni Kagera
4.HUMPREY S/O LEONARD Miaka 34, mlinzi, mkazi wa Mburahati
5.FRANK S/O CHARLES Miaka 31 mfanyabiashara, mkazi wa Sinza
6.ABDALLAH S/O YUSUPH, Miaka 34, mfanyabiashara, Mkazi wa Sinza
7.BAKARI S/O BAKARI, Miaka 31, mfanyabiashara, mkazi wa Mbezi, Kimara.
Aidha watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria
0 comments: