Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
4:25 AM
OPERESHENI
ya kukamata pikipiki maarufu kama bodaboda zinazoingia katikati ya Jiji
la Dar es Salaam, imedaiwa kuhatarisha maisha ya watu kutokana na
polisi kutozingatia usalama wa wapanda pikipiki hao wanapowakamata na
kuwasababishia ajali.
Baadhi
ya waandishi wa habari walishuhudia kamata kamata hiyo iliyolalamikiwa
na baadhi ya wananchi katika makutano ya Mtaa wa Garden na Azikiwe,
Manispaa ya Ilala jana, huku ikisimamiwa na Kamanda C.N Maro.
Ajali
hizo zimekuwa zikitokea kutokana na polisi kuwakimbiza wapanda pikipiki
hao na kuwavuta kwa nguvu kutoka kwenye pikipiki huku wakiwa kwenye
mwendo kasi pindi inapotokea mhusika amekataa kusimama.
Baada
ya kukamatwa, mhusika hufungwa pingu kwa kuunganishwa na pikipiki yake
na kuamriwa akae chini, kitendo kilicholalamikiwa, kwamba ni ukiukwaji
wa haki za binadamu.
Katika
eneo hilo, zilikamatwa zaidi ya pikipiki 50, kati ya hizo zikiwemo za
baadhi ya kampuni na raia wa kawaida, ambazo zilikuwa na vibali vya
kuingia katikati ya jiji.
Hata
hivyo, polisi hao walikataa kuwasikiliza kwa madai hawana taarifa kuwa
kuna vibali vinavyoruhusu pikipiki kuingia katikati ya jiji.
Polisi
hao, pia walimkamata na kumfunga pingu mtu mmoja ambaye jina lake
halikuweza kupatikana mara moja, kutokana na kuhoji utaratibu uliokuwa
ukitumika kuwa haukuzingatia usalama wa wahusika ambao ungeweza
kuwaletea madhara.
Katika
hali isiyotarajiwa, polisi hao walimgeuzia kibao mtu huyo kuwa alimpiga
askari na kumfanya ashindwe kufanya kazi yake wakati haikuwa kweli.
Waandishi
walipofika katika eneo hilo kutaka kupatiwa ufafanuzi kuhusu askari hao
kuendesha operesheni hiyo kikatili huku wakiwa peke yao bila mgambo wa
jiji, Kamanda Maro alikataa kujibu na kuwaamuru kuondoka.
“Ondokeni tufanye kazi yetu, haiwahusu,” alisema.
Alipotafutwa
Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kabwe, alisema kuhusu operesheni hiyo, mkoa
umekubaliana iendelee na hilo la kufungwa pingu inategemea mhusika
alivyokuwa akitii sheria.
Pia,
alishangaa kusikia kukamatwa kwa mtu aliyekuwa akihoji ukiukwaji wa
taratibu za ukamataji, na kusema hata hivyo atawasiliana na Kamanda wa
Kanda Maalum, Kamishna Seleman Kova, ili kupata ufafanuzi kuhusu tukio
hilo
chanzo:sophie
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: