ADEN RAGE APATA AJALI DODOMA
Na Mdau Wetu
WABUNGE kutoka mkoa wa Tabora akiwemo Mbunge wa Viti Maalum Munde Tambwe (34) na Mbunge wa Tabora mjini Ismail Rage (60) wote wa CCM wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Dodoma baada ya kupata ajali leo wakiwa wanatokea Tabora kuelekea Bungeni mjini Dodoma.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Chigongwe katika Manispaa ya Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Ezekiel Mpuya alisema wabunge hao wamepokelewa pamoja na abiria wengine waliokuwa wamewabeba kwenye gari yao ambao ni Mwanahamisi Ramadhani (14) na John hoya (32). majira ya saa sita mchana.
Alisema baada ya vipimo imeonesha Munde amevunjika bega la kushoto na amepata majeraha kichwani huku Rage akiwa ameteguka bega la kushoto.
Dk.Mpuya alisema majeruhi wengine wawili majibu ya vipimo bado yanasubiriwa.
"Majeruhi wote hali zao zao siyo mbaya na wanaendelea na matibabu,na kwamba baada ya muda wa siku chache watarejea katika afya zao za kawaida.
Akisimulia namna ajali ilivyokea Rage alisema,dereva wa hari yake alitaka kulipita gari la lililokuwa mbele yao na kusababisha ajali hiyo.
"Mbele yetu kulikuwa na gari ambalo lilikuwa linatembea nje ya barabara,sasa dereva wa gari yangu alipotaka kulipita lile gari ghafla waliona imeingia barabarani na wakati huo mbelw kulikuwa na gari lingine linakuja na hatimaye dereva wangu akaelekea kulia zaidi na kuacha njia,
"Dereva amefanya jitihada kubwa sana na tumashukuru Mungu ,maana ukiliona gari lilivyo ,huwezi kuamini kama tumetoka katika hali tulizonazo." alisema Rage
0 comments: