Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
7:16 AM
Habari
zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba, mwimbaji maarufu wa nyimbo za
injili hapa nchini, Bahati Bukuku amenusurika kifo baada ya gari
alilokuwa akisafiria kupata ajali mbaya katika eneo la Kongwa, mkoani
Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu
wa chanzo chetu cha habari, mwimbaji huyo alipata majeraha makubwa
sehemu mbalimbali mwilini na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinadhaniwa
kuwa ni mwendokasi.
Chanzo
hicho hakijaweza kueleza zaidi kwamba Bukuku alikuwa akielekea ama
kutoka mkoani Dodoma na kama ndani ya gari hilo kulikuwamo na abiria
wengine.
Pia haikuweza kufahamika mara
moja kama mwimbaji huyo alikuwa akiendesha mwenyewe gari hilo, ingawa
kilithibishwa ajali hiyo na kwamba Bukuku alijeruhiwa vibaya.
Endelea kuperuzi blogu hii kwa habari zaidi ya tukio hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: