Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
5:12 AM
Mbunge
wa Jimbo la Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli akipeana mikono na Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
walioamua kujiunga na chama hicho mara baada ya Mbunge huyo kufanya
Mkutano mkubwa wa hadhara katika kijiji cha Nyabugela, kata ya Mganza
katika Wilaya ya Chato leo.
Mbunge
wa Jimbo la Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli kihutubia mamia ya wakazi wa kata ya Mganza katika Wilaya ya
Chato leo.
Wananchi
wa Kata ya Mganza wakimfurahia Mbunge wa Jimbo lao la Chato Mheshimiwa
Dkt. John Magufuli wakati akiwahutubia na kuwasisitiza wafanye kazi kwa
bidii ili waweze kujiletea Maendeleo.
Mbunge
wa Jimbo la Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe
Magufuli akiwapokea wanachama wapya zaidi ya 100 walioamua kujiunga na
Chama cha Mapinduzi CCM mara baada ya mbunge huyo kumaliza hotuba yake.
Wanachama
wapya wa Chama cha Mapinduzi kata ya Mganza wakila kiapo mbele ya
Mbunge wao Mheshimiwa Dkt.John Magufuli ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi
baada ya kukabidhiwa kadi za uanachama hivi leo.
Waziri
wa Ujenzi ambaye pia ni mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt John Pombe
Magufuli amezidi kuongeza idadi ya wanachama wapya katika Chama cha
Mapinduzi (CCM) baada ya mkutano wake wa siku moja kuzoa wanachama wapya
376.
Hali
hiyo imekua pigo kubwa kwa vyama vingine vya siasa kwasababu katika
muda mfupi wa mikutano ya Mbunge huyo idadi ya wanachama waliotoka
katika vyama vya upinzani imezidi kuongezeka.
Katika
mikutano hiyo iliyofanyika katika vijiji vya Nyisanzi, Kasenda na
Muganza. Dkt. Magufuli alieleza jinsi alivyotekeleza ahadi mbalimbali
zilizomo kwenye za Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika kutatua kero
mbalimbali za wanachi.
“Mlinichagua
kwa kura nyingi sana hapa na mimi lazima nionyeshe mfano katika
kuwatumikia na naahidi vitu vyote nilivyoahidi nimetekeleza kwa sehemu
kubwa kuanzia kwenye shule, huduma za afya, barabara, maji na umeme”
alisema Dkt. Magufuli
Katika hatua nyingine Dkt. Magufuli aliwaasa vijana kufanya kazi kwa bidii na kuacha kudanganywa na wanasiasa uchwara.
“Nawaambia
hakuna kitu cha bure, wala hakuna mtu atakayewaletea kitu chochote kama
hamtajishughulisha, mfanye kazi muache maneno ya kukaa vijiweni”
alisema Dkt Magufuli
Akizungumza
huku akishangiliwa na umati wa watu, Dkt. Magufuli aliwataka wakazi wa
Muganza kufanya kazi kwa bidii na kutumia fursa za kiuchumi zinazoanza
kufunguka katika kata hiyo.
“Hapa
Muganza ndipo linajengwa lango kuu la watalii kuelekea hifadhi ya Taifa
ya Rubondo, hivyo ni bora mkajianda mapema na fursa hii, mkikaa bila
kufanya kazi fursa hizi zitawapita tu” alisema Dk. Magufuli
Aidha, Mbunge huyo wa Chato pia alisema watanzania wanatakiwa kudumisha Amani iliyopo isije kupotea kwani gharama yake ni kubwa.
Waziri
Magufuli alitolea mfano wa nchi za Misri, Libya na Iraq jinsi
zilivyokuwa na Amani hapo zamani lakini sasa hivi hali yake ni mbaya
watu wanauana kila muda.
“Wakataeni
wanasiasa wanaohubiri siasa chafu za kuvuruga Amani, na eti kudai hadi
kieleweke vinginevyo damu itamwagika, akija mtu kama huyo mwambieni
amwage damu yake kwanza, msimkubali kwani atawapoteza” alisisitiza Dkt.
Magufuli.
Katika
hatua nyingine Waziri Magufuli amewaahidi wakazi wa Muganza kuwa
Serikali itamalizia kipande cha barabara kisichozidi kilomita tatu
katika kata hiyo, kwani ni ahadi ya Mhe. Rais na tayari Wizara ya Ujenzi
kwenye bajeti yake ya mwaka huu wa fedha 2014/15 imetenga kiasi cha sh.
50.mil kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mwanzo ya ujenzi wa barabara
hiyo.
“Serikali
ya CCM imeahidi na itatekeleza ahadi yake, tumejenga barabara kila kona
ya nchi hatuwezi kushindwa kumalizia kipande hichi kidogo, alisema Dkt.
Magufuli .
Pia katika mikutano hiyo waziri Magufuli alitoa michango mbalimbali katika shule na vituo vya afya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: