DC KAHAMA AWATAKA TANESCO KUONDOA UMEME WA LUKU KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA,

 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya ameuagiza uongozi wa halmashauri ya mji wa kahama kuhakikisha wanauondoa mara moja umeme wa luku katika hospitali ya wilaya na badala yake watumie ule wa mita uliokuwa ukitumika siku zote za nyuma.
 
Agizo hilo amelitoa jana wakati akiongea na watumishi wa hospitali ya mji huo ambapo amedai umeme wa Luku haufai katika matumizi ya kuhudumia wagonjwa kwa kuwa Luku ikiisha unakatika hata wakati Madaktari wakiwa katika upasuaji
 
Aliwaagiza viongozi wa hospitali hiyo mara tu umeme wa luku walionunua ukiisha waiondoe mara moja mita hiyo na kisha wairudishe ile ya zamani ambayo haitumii Luku
 
Alisema pamoja na mabadiliko ya kitechnologia katika matumizi ya umeme  ikiwa ni pamoja na Shirika la umeme Tanzania Tanesco kuwa katika mabadiliko ya matumizi ya mita lakini Luku haifai katikaa matumizi ya kuhudumia wagonjwa katika hospitali
 
Halmashauri hiyo ya mji kupitia mkurugenzi wake Felix Kimario ilifanya mabadiliko ya matumizi ya umeme katika hospitali hiyo kwa lengo la kuboresha  lakini imekuwa ni tatizo kwa wagonjwa Luku inapokwisha wakati madaktari wakiwa katika upasuaji ambao huzimikiwa mwanga gafla .

0 comments: