Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
12:36 AM
Sheikh
wa Msikiti wa Qiblatan, Sood Ally Sood (37), uliopo Kilombero jijini
Arusha amelipuliwa na bomu la kurusha kwa mkono akiwa nyumbani kwake
wakati wakila daku hapa akiwa amelazwa katika Hospitali ya Mt. Meru,
alijeruhiwa miguuni na mapajani.
Ads by MediaAdsAd Options
Sheikh
wa Msikiti wa Qiblatan,Sood Ally Sood (37) uliopo Kilombero jijini hapa
amejeruhiwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono alipokuwa akila daku
nyumbani usiku wa kuamkia jana.
Pamoja na Sheikh Sood, mtu mwingine aliyekuwa nyumbani kwake,aliyetajwa
kwa jina la Muhaji Kifea (38) mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam pia amejeruhiwa katika tukio hilo na wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa matibabu.
Sheikh
alijeruhiwa miguu yake yote na mapajani huku Kifea akipata majeraha
makubwa miguuni na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote.
Akizungumza
hospitalini hapo, Sheikh, Sood alisema tukio hilo lilitokea nyumbani
kwake eneo la Majengo ya chini, usiku wa kuamkia jana saa 5:00 wakati
yeye pamoja na mgeni wake walikuwa wakila chakula sebuleni.
“Nikiwa
sijui hili wala lile nilishtushwa na mlipuko ulioambatana na vyuma
mbalimbali vilivyokuwa vikiruka hewani ambapo bomu hilo linaelezwa kuwa
ni guruneti lililorushwa kupitia dirishani baada ya watu wasiofahamika
kufanikiwa kuvunja kioo cha dirisha la chumba tulichokuwamo,” alisema
Sheikh Sood.
Alidai
anawajua waliotekeleza shambulio hilo kwa sababu amekuwa akipokea
vitisho kutoka kwa watu anaowafahamu na tayari alikuwa ametoa taarifa
kwa vyombo vya dola.
Alisema kuwa siku tatu
kabla ya tukio hilo alikoswakoswa kupigwa risasi na watu wasiofahamika
wakati akitoka msikitini na akatoa taarifa Kituo Kikuu cha Polisi jijini
Arusha kuhusu tukio hilo. Sood anasema kuna baadhi ya vijana
anawatuhumu juu ya matukio hayo.
Sheikh huyo ambaye ni Kiongozi wa dhehebu la Answar sun
Kanda ya Kaskazini amekuwa akitofautiana na waumini wenzake kutokana na
msimamo wake wa kutokukubaliana na baadhi ya waumini wenye msimamo
mkali wa msikiti huo.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alikemea matukio ya mabomu
yanayolitikisa Jiji la Arusha katika siku za karibuni na kuviagiza
vyombo dola kufanya uchunguzi wa kina kubaini wahusika wote ili hatua za
kisheria zichukuliwe dhidi yao.
“Uchunguzi
wa awali unaonyesha tukio hili limetekelezwa na watu walio karibu na
Sheikh. Polisi wanaendelea na uchunguzi kwa sababu baadhi ya watu
wanaotajwa kuhusika kwenye tukio hili pia ni miongoni mwa watuhumiwa
kwenye matukio mengine ya milipuko ya bomu Arusha,” alisema Mulongo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatusi Sabasi alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kueleza kuwa majeruhi wanaendelea vyema huku polisi
wakiendelea na uchunguzi wa kina kuwabaini wahusika.
Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema alielezea kusikitishwa na matukio ya
milipuko ya mabomu Arusha na kuliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi
wa kina kuwakamata wahusika bila kujali vyeo, nyadhifa, dini, itikadi
wala rangi zao.
“Arusha
tunapita katika kipindi kigumu sana. Kwanza tulishuhudia mlipuko wa
bomu kanisani, ikafuatiwa na lile la mkutano wa hadhara wa Chadema,
kabla ya mwingine kulipuka kwenye baa na sasa nyumbani kwa Sheikh,”
alisema Lema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: