Serengeti Breweries Limited (SBL) yatangaza uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa bodi ya wakurugenzi
Mheshimiwa Nehemia Mchechu kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba la Taifa( NHC) . Bw. Mchechu ana uzoefu mkubwa katika masuala ya fedha na usimamizi. Hapo awali alishika nafasi muhimu katika sekta ya benki , hasa kama Mkuu wa Masoko Kimataifa na mkurugenzi msaidizi benki ya Standard Chartered, na kuwa Mkurugenzi Mtendaji benki ya Commercial Bank of Africa Tanzania (CBA) .
Mheshimiwa Mchechu ana Shahada ya Biashara (Fedha) na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Yeye pia ni Rais wa Umoja wa wanfunzi waliomaliza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Biashara na mwanachama wa ACI – Financial Market Association Tanzania.
Miongoni mwa nafasi nyingine muhimu, Mheshimiwa Mchechu pia ni Mkurugenzi na mwanachama wa CEORT na pia ni Mkurugenzii wa TIC.
SBL inachukua fursa hii kumkaribisha na kumpongeza Mwenyekiti wake mpya wa bodi na kuwashukuru mwenyekiti wa bodi Mheshimiwa Bomani kwa mchango wake bora na wa kipekee wakati wa uongozi wake.
0 comments: