Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
7:48 AM
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wanachama wa CCM wa
Tawi la STEMMUCO mkoani Mtwara wakati wa sherehe za kuwaaga wanachama
wa CCM waliohitimu masomo yao katika Chuo cha SAUT ambapo aliwaambia
wasomi washiriki katika kukisaidia chama hasa katika kuboresha sera
mbali mbali.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani akizungumza
wakati wa sherehe za kuwaaga wanachama wa CCM Tawi la STEMMUCO mkoani
Mtwara ambao wamehitimu masomo katika Chuo cha SAUT ,Mwenyekiti
aliwaeleza wanafunzi hao kuwa CCM ni chama pekee kinachoweza kuwavusha
kutoka hapa walipo na kusonga mbele.
Katibu
wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akizungumza wakati wa
sherehe za kuwaaga wanachama wa CCM Tawi la STEMMUCO mkoani Mtwara ambao
wamehitimu masomo katika Chuo cha SAUT ambapo alisisitiza wasomi kufanya tafiti zao kabla ya kuchagua chama gani cha siasa kinaweza kuwasaidia.
Baadhi
ya wanachama waliohitimu kutoka chuo cha SAUT wakifuatilia kwa makini
hotuba kutoka kwa viongozi wao wakati wa sherehe za kuwaaga rasmi
zilizofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste COCO Beach Mtwara
Mwajuma Abas Nasombe na Zena Ibrahim wakiimba shairi maalum linalohusu CCM
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiimba nyimbo za hamasa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akionyesha juu moja ya kadi
za Chadema zilizorudishwa kisha wanachama hao kujiunga na CCM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: