'Mwanamke
wa Nigeria aliyejitambulisha kwa jina la Mercy James amesimulia tukio
la ajabu la kujifungua salama mtoto wa kike baada ya kuwa mjamzito kwa
kipindi cha miaka 14. Mtoto aliyeamua kumuita ‘Miracle’
Kwa
mujibu wa Vanguard, Mercy alieleza kuwa alianza kujisikia dalili za
ujauzito miaka 14 iliyopita lakini awali dalili hizo zilikuwa
zinabadilika na mara nyingine anaingia katika hedhi kwa siku moja,
lakini hali ilianza kuwa serious miaka miwili baadae alipoenda hospitali
na kuhakikishiwa kwa vipimo kuwa ni mjamzito. Nilienda
tena kwa tabibu miaka miwili baadae na kumlalamikia kuhusu maumivu
niliyokuwa nayapata, aliniambia tena kuwa sina tatizo la tumbo na kwamba
huo ulikuwa ujauzito. Alinishauri niendelee na maombi ili Mungu
aniepushe na mikono ya shetani.
Mercy alisimulia.
Anaeleza kuwa alikuwa anatumia madawa mengi ya kutibu magonjwa ya tumbo lakini hali yake haikubadilika.
Hali
iliendelea hivyo hadi ilipofika June 7 mwaka huu ambapo alienda tena
katika hospitali hiyo akiwa analalamika na kusikia kila dalili za kitu
kutaka kutoka mwilini mwake, lakini hakufahamu kuwa hiyo ingekuwa siku
ambayo angejifungua mwanae wa kike, ‘Miracle’.
Kisha
Mungu aliamua kunifuta machozi. Katika siku niliyojifungua mwanangu wa
kike, mwanzo nilihisi ni minyoo inataka kutoka kwenye mwili wangu bila
kufahamu kuwa yule alikuwa mtoto. Hivi ndivyo nilivyomwambia mkunga.
Lakini baada ya kunipima alianza kuniambia nisukume. Nilimpotezea.
Baadae nikaishiwa fahamu kama dakika 15 na nilipopata fahamu, nilisikia
mtoto Analia. Nilishangaa sana na kuchanganyikiwa nilipomuona mwanangu.
Sikuweza kuamini macho yangu.
Mercy aliendelea kusimulia tukio hilo.
Naye
tabibu wa hospitali ya kanisa la ‘Celestial Church Of Christ, Parokia
ya Kadoso ambapo Mercy alijifungulia, aliyetajwa kwa jina la Ajegunle
aliliambia Vanguard kuhusu hatua zote alizopitia hadi kujifungua mwanae
huyo na jinsi yeye binafsi kama mkunga alivyohusika.
Marafiki na ndugu wa mwanamke huyo walitoa ushuhuda pia kwa gazeti la Vanguard la Nigeria kuhusu tukio hilo la kushangaza.
0 comments: