WAREMBO WA REDD'S MISS TANZANIA KUKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI LEO
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:56 AM
Na Mwandishi Wetu
WAREMBO
30 wanaowania taji la Redd’s Miss Tanzania, leo wanatarajiwa kukutana
rasmi na waandishi wa habari, ili kila mmoja kutoa mtazamo wake shughuli
itakayofanyika katika hoteli ya Giraffe iliyopo Kunduchi, Dar es
Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino walio waandaaji
wa Redd’s Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema, mkutano kati ya
waandishi wa habari na warembo ni muhimu kuwajengea uwezo zaidi wa
kujiamini.
“Washiriki
hao wataulizwa maswali mbalimbali na waandishi wa habari na wao
wataeleza mtazamo wao kuhusu Redd’s Miss Tanzania, hatutawafunga, wao
waandishi watakuwa huru kila mmoja kumuuliza mshiriki yoyote swali
analotaka,” alisema.
Jana
washiriki hao walikuwa na semina maalumu kati ya washiriki hao na
waandaaji wa mashindano haya ambao ni Kampuni ya Lino International
Agency Limited.
Baada
ya kukutana na waandishi wa habari leo, warembo hao wanatarajiwa kuanza
ziara maalumu ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa
lengo la kuhamasisha utalii wa ndani.
Warembo
hao watakuwa kambini kwa muda wa siku 30 wakipata mafunzo mbalimbali
yatakayotolewa na wataalamu kutoka katika sekta mbalimbali kama vile
afya, ajira, ujasiriamali, uwekezaji na sekta ya utalii.
Brigitte Alfred ndiye anayeshikilia taji hilo kwa sasa, baada ya kufanikiwa kulitwaa mwishoni mwa mwaka jana.
Meneja
wa Redd’s, Victoria Kimaro naye alisema kama wadhamini wapo tayari
kuhakikisha shindano hilo linafanikiwa zaidi mwaka huu kuliko kipindi
chote kile.
Kinywaji cha Redd’s Original kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzan
You might also like:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: