USHURU UNAOKUSANYWA HAPA NI PESA TOSHA ZA KUTENGENEZA MAZINGIRA YA COCO BEACH, ETI WADAU MAGARI YOTE HAYA KILA MOJA BUKU NI SH. NGAPI??
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 8:08 AM
Haya
ni sehemu tu ya magari yanayoegeshwa kwenye Ufukwe wa Coco Beach siku
za wikiendi, ambapo kila garo moja hutozwa ushuru wa Sh. 1,000/= kila
moja na moja ya Kampuni inayojiita Mtaa wa Oysterbay.
Lakini
cha kushangaza wakusanyaji wa ushuru huo wanashindwa kuelezea mapato na
matumizi ya pesa hizo zinazokusanywa kila siku kuanzia jumatatu hadi
jumapili, huku wakusanyaji hao wakiogopa kuchukua ushuru huo kwa baadhi
ya magari kwa kuhofia kuhojiwa kuhusu uhalali wa ukusanyaji wa ushuru
huo.
Vijana
hao wanaokusanya ushuru hulazimika kumuangalia mtu usoni kabla ya
kumface na kumuomba kulipia maegesho hayo yasiyokuwa na mabadiliko
yeyote wala kufanyiwa ukarabati kutokana na pesha hizo zinazokusanywa.
Ingekuwa
ni vyema wahusika wakabuni ulaji huo kwa kutengeneza mazingira hayo
kutengeneza maegesho bota ya magari kwa mpangilio, kufanya usafi na hata
kuboresha mazingira hayo kwa ujumla.
Ushuru
huu si kwa wenye magari pekee kwani hata wauzaji wa mihogo, Viazi,
soda, Clips nao pia hutoa ushuru wa Sh. 5,000/= kila mmoja ambapo wao
wanafaidika na huduma ya kuzolewa taka zao tu inayotolewa na Manispaa.
Nyomi la magari kama hivi, halafu pesa hazijulikani zinapokwenda......
Hawa
ni sehemu tu ya watu wanaofika kwenye eneo hilo siku za wikiendi kwa
ajili ya kupumzika na kupata vitafunwa kama mihogo na viazi vya
kukaanga, huku wakipunga upepo wa bahari.
Wauzaji wakiandaa biashara zao.......
Wakazi wa maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam, wakiwa eneo hilo.
Ni kupunga upepo kwa kujinafasi.......
Mmoja kati ya wafanyabiashara wa eneo hilo wakiandaa biashara zao.......
You might also like:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: