BAYERN MUNICH WAIFUMUA MAN CITY 2-1 FAINALI KOMBE LA AUDI, ILA BAO LA NEGREDO SHIKA ADABU YAKO WEWE!
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 8:16 AM
IMEWEKWA AGOSTI 2, 2013 SAA 1:19 ASUBUHI
MSHAMBULIAJI Edinson Cavani anaweza
kuwa mchezaji aliyekuwa akitakia mno Manchester City, lakini hawawezi
kujutia kumkosa baada ya Alvaro Negredo kufunga bonge la bao Uwanja wa
Allianz Arena wakati hiyo ikilala 2-1 mbele ya wenyeji Bayern Munich
katika fainali ya Kombe la Audi.
Wakati Cavani akifuata ofa ya Paris St
Germain, Negredo amedhihirisha makali yake ambayo City inapaswa
kujivunia kuwa na mpachika mabao huyo.
Mabao ya mabingwa wa Ulaya yalifingwa
na Muller kwa penalti dakika ya 65 na Mandzukic dakika ya 72, wakati la
City lilipatikana dakika ya 61, mfungaji Negredo.
Kikosi cha Bayern Munich
kilikuwa: Neuer, Lahm (Weiser 90), Dante, Martínez, Alaba,
Thiago/Mandzukic dk57, Schweinsteiger, Kroos/Rafinha dk59,
Robben/Shaqiri dk57, Ribéry na Müller,
Manchester City:
Pantilimon, Zabaleta, Kompany, Boyata, Clichy, Fernandinho, Nasri,
Milner, Barry/Toure dk46, Jovetic/Navas dk46, Negredo/Dzeko dk75.
Mario Mandzukic (wa pili kushoto) akimtungua Costel Pantilimon kuipa Bayern ushindi wa 2-1
Mchezaji wa Bayern, Toni Kroos akipambana na mchezaji mpya wa City, Alvaro Negredo
Dedryck Boyata akipambana na winga Mfaransa wa Bayern Munich, Franck Ribery
Domo: Kocha Mkuu wa Bayern Munich, Pep Guardiola akiingalia timu yake jana
Manuel Neuer akimdhibiti Samir Nasri
Alvaro Negredo akishangilia kuifungia bao la kuongoza Manchester City
Thomas Muller akiifungia kwa penalti Bayern Munich
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: