Rais Wa Marekani Barack Obama Akutana na Kuhutubia watendaji wakuu(CEO) wa Makampuni mbalimbali yaliyowekeza Afrika Juu ya Kuimarisha Fursa Za Ushirikiano Kati ya Marekani na Afrika katika Uwekezaji Kwenye Sekta Mbalimbali za Maendeleo.
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:04 AM
Rais
wa Marekani Barack Obama akiwahutubia wafanyabiashara jana jijini Dar
es salaam juu ya mpango wa Nchi yake wa kufungua milango ya ushirikiano
na uwekezaji kwa Nchi za Afrika Mashariki katika sekta mbalimbali na
hivyo kuongeza kiwango cha bidhaa ya Afrika Mashariki zinazoingia
nchini Marekani.
Rais
wa Marekani Barack Obama akiwa katika mkutano jana jijini Dar es
salaam wa kujadiliana na watendaji wakuu(CEO) wa Makampuni mbalimbali
yaliyowekeza Afrika juu ya kuimarisha fursa za ushirikiano kati ya
Marekani na Afrika katika uwekezaji kwenye sekta mbalimbali za
maendeleo.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es Salaam
---
Na Eleuteri Mangi—MAELEZO.Dar es salaam
Serikali
ya Marekani imeahidi kufungua ukurasa mpya kwa Nchi za Afrika Mashariki
kwa kuongeza uwekezaji katika sekta mbalimbali ili kuinua uchumi wan
chi hizo.
Kauli
hiyo imetolewa jana mjini Dar es salaam na Rais Barack Obama kwenye
hotuba yake kwa wafanyabiashara wakati wa ziara yake ya siku mbili
nchini Tanzania.
Alisema
kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza kiwango cha bidhaa kutoka Nchi za
afrika Mashariki kuingia nchini Marekani na hivyo kuimarisha ushirikiano
wa kibiashara na kiuchumi kwa manufaa ya pande zote.
“Sasa
ni wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwekeza nchini Marekani ili
kuongeza mauzo yake nchini Marekani hadi ifike asilimia 40,” alisema
Rais Obama.
Aliongeza
kuwa pia ushirikiano huo unapaswa kuboresha utoaji wa mizigo katika
bandari ya Dar es salaam na Mombasa kwenda nchi zisizo na bandari ili
kuinua uchumi wa eneo hilo kwa kupunguza muda wa mizigo kukaa
bandarini.
Akizungumzia
hotuba ya Rais Obama Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye viwanda nchini
(CTI) Felix Mosha alipongeza hotuba hiyo kwa kufungua ukurasa mpya kwa
nchi za Afrika na Marekani kwa kuonyesha kuwa wakati wa kutegemea
misaada umepitwa na wakati badala yake ni kushirikiana katika uwekezaji.Katika mkutano huo kiasi cha wafanyabiashara 170 walihudhuria mkutano huo .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: