Alisema Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka
mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye
namba za usajili T 911 BUG aina ya Toyota Spacio ambapo baada ya kusimamishwa
katika eneo hilo wakitokea Kyela kuelekea Jijini Mbeya.
Alisema baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi
ovyo ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo
waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini
Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.
Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha
mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki
risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na
risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.
Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza
kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika,
Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya.
Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana
maramoja ambapo miili hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito
kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili
wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.
Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu
kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.
Picha na Mbeya yetu
0 comments: