MADAKTARI BINGWA WA MOI KWA KUSHIRIKIANA NA MADAKTARI BINGWA HOSPITALI YA NYANGAO MKOANI LINDIA WAWAFANYIA UPASUAJI WAGONJWA 1500
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 2:06 PMWATAALAM WA AFYA NCHINI WAPATIWA MAFUNZO YA KIMATAIFAA JINSI KUFANYA KIPIMO CHA MOYO KWA KUTUMIA MASHINE YA ECHOCARDIOGRAM (ECHO)
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 2:08 AMMkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi kwa kutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO) yanayoendelea katika Taasisi hiyo Jijini Dar Es Salaam. Mafunzo hayo yaliyoudhuriwa na wataalam wa afya zaidi ya 100 yamefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.
Na: Genofeva Matemu – Dar es Salaam
19/08/2022 Wataalam wa afya zaidi ya 100 kutoka hospitali binafsi
na hospitali za umma wameshiriki mafunzo yakimataifa ya siku mbili ya upimaji wa
jinsi moyo unavyofanya kazi kwa kutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO) ambayo
yamefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.
Akizungumza na waandhishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mafunzo
hayo leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema kuwa mafunzo hayo yanatolewa na wakufunzi na
wabobezi wakuu wa magonjwa ya moyo kutoka nchini Marekani.
Prof. Janabi alisema kuwa lengo la mafunzo hayo nikuongeza ujuzi
kwa wataalam wa afya ili kusaidia na kupunguza wagonjwa ambao wanaingia gharama
kutoka mikoani kwenda JKCI kwa ajili ya kufanyiwa kipimo cha Echo kwani wakiweza
kuwagundua katika maeneo yao ya kazi wataweza kuchagua wagonjwa wanaohitaji kufanyiwa
matibabu zaidi na kuwatuma JKCI.
“Tumekua tukifanya mafunzo kama hayo huko nyuma lakini kwa kutumia
wataalamu wetu wa ndani ndio maana leo tunasema haya ni mafunzo yetu ya kwanza
yakimataifa kwasababu tuna wabobezi na wataalam zaidi katika uchunguzi wa jinsi
moyo unavyofanya kazi (ECHO) kutoka nchini Marekani”,
“Kwetu sisi wataalam wakutoa huduma za matibabu ya moyo,
hatuwezi kufanya upasuaji wa aina yoyote bila kufanya kipimo cha Echo hivyo ujuzi
tutakaoupata hapa utasaidia zaidi kuboresha huduma zetu na kuchagua wagonjwa wapi waende kwenye upasuaji
na wangapi wanaweza kutumia dawa bila ya kufanyiwa upasuaji”, aliseama Prof.
Janabi
Prof. Janabi alisema kuwa mafunzo ya upimaji wa jinsi moyo unavyofanyakazi
kwa kutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO) yataendelea kutolewa kila mwaka kwa
wataalam wote wa afya bila kubagua waliopo katika hospitali za umma na zile za binafsi
ili kujifundisha mbinu mpya za kugundua matatizo ya moyo awali kabla ya tatizo kuwa
kubwa.
Mshiriki wa mafunzo hayo ambaye ni Mbunge wa viti maalum Mhe.
Dkt. Alice Kaijage alisema kuwa ameshiriki mafunzo ya upimaji wa jinsi moyo unavyofanya
kazi kwa kutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO) ili aweze kupata mbinu mpya na
zakisasa katika kutoa huduma za matibabu ya moyo.
“Nikiwa bungeni tuna kituo cha afya hivyo kwanjia moja ama nyingine
naweza kusaidiana na wenzangu kama mtaalamu kupima moyo unavyofanya kazi kwa wagonjwa
wanaofika katika kituo hicho lakini pia kupitia taaluma yangu natakiwa kuongeza
ujuzi ili niweze kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia”
Kwa upande wake Mkufunzi kutoka Taasisi ya Piedmont Health
iliyopo Atlanta Georgia nchini Marekali Dkt. Mani Vannan alisema kuwa anaamini katika
mafunzo ya mara kwa mara katika taaluma ya afya na nimoja ya matamanio yake kuona
wataalam wa afya wanashiriki mafunzo ya kuongeza taaluma zao kila wanapopata fursa.
“Naamini Taasisi hii inamisingi mizuri katika taaluma ya upimaji
wa jinsi moyo unavyofanya kazi kwa kutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO),
madhumuni ya mafunzo haya nikuifanya nchi hii kuwa kituo cha ubora katika utoaji
wa huduma za kibingwa za vipimo na matibabu ya moyo”, alisema Dkt. Mani
Naye Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi katika Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delila Kimambo alisema kuwa kipimo cha
kuangalia jinsi moyo unavyofanyakazi ni moja ya huduma za tiba shirikishi ambayo
nimuhimu kwa mtaalam wa afya kujua matatizo aliyonayo mgonjwa na kumpa mwelekeo
wa huduma gani mgonjwa anastahili kupewa.
“Mgonjwa yeyote wa moyo nilazima afanyiwe kipimo cha
kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO), ni kipimo muhimu ambacho wataalam
waliopo hapa leo wanapaswa kukifahamu kwa undani zaidi ndio maana tumeandaa mafunzo
haya ili tuwakumbushe na kuwafundisha waweze kutoa huduma hiyo katika ubora zaidi”,
“Unapofanya kipimo cha Echo vyema zaidi unamsaidia mgonjwa kupata
huduma bora zaidi, kumpa taarifa sahihi itakayomsaidia katika matibabu yake pamoja
na kujua tatizo lake kama linahitaji dawa ama upasuaji”, alisema Dkt. Delila
TAASISI YA MUSLIM WORLD LEAGUE INATEKELEZA MPANGO WA KWANZA WA UPASUAJI WA MOYO WA "LAPAROSCOPIC" NCHINI TANZANIA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:40 AMDar Es Salaam:
Taasisi ya Muslim World League itazindua mpango wa hali ya juu wa matibabu katika upasuaji wa moyo wa watu wazima katika Kituo cha Moyo JKCI katika mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam, kuanzia tarehe 14 hadi 19 Agosti, kwa ushirikiano na Wizara ya Afya ya Tanzania na Kituo cha Upasuaji wa Moyo.
Hayo yamesemwa na Mkurugezi Taasisi ya Muslim World League Nchini Tanzania, Hassan Katungunya wakati wa ugeni wa Naibu Waziri wa Afya kutoka nchini Malawi Mhe. Enock Phale kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kuangalia mifumo ya Tehama inayotumika katika uendeshaji wa Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Katika kutekeleza mpango huo teknolojia bora na za kisasa zaidi zitatumika na kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, "roboti" maalumu katika upasuaji wa moyo itaanzishwa. Hii husaidia kupunguza kukaa kwa mgonjwa hospitalini, pamoja na kupunguza hatari ya kuambukizwa na kasi ya mgonjwa kurudi kwenye maisha ya kawaida ndani ya kipindi kifupi.
Mpango huu ni mpango maalumu wa kwanza kufanyika nchini Tanzania kwa kutumia vifaa vya hali ya juu na chini ya usimamizi wa timu ya madaktari bingwa na madaktari bingwa wa upasuaji inayoongozwa na Prof. Othman Al-Uthman.
Timu ya upasuaji ya chama itafanya operesheni ngumu kwa kikundi cha wagonjwa waliochaguliwa kwa uangalifu, baada ya kufanya vipimo vingi ili kuhakikisha afya zao na hitaji lao la kufanyiwa upasuaji huu.
Miradi ya afya inawakilisha kipaumbele cha juu kwa Taasisi ya Muslim World League, kwani inatoa huduma kamili za afya kwa vikundi dhaifu na masikini kote ulimwenguni, pamoja na juhudi na rasilimali zake za kuinua ubora na ufanisi wa huduma za afya katika nchi nyingi, kwa kushirikiana na mamlaka rasmi zinazohusika ndani yao.
Taasisi ya Muslim World League pia inatekeleza programu adimu na zenye thamani ya juu za afya, kwani ilitekeleza mipango mingi kama hiyo, ambayo ya mwisho ilikuwa nchini Mauritania mwaka jana.
Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Molle akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya Nchini Malawi Mhe. Enock Phale katika Taasisi ya Moyo ya JKCI kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kuangalia mifumo ya Tehama inayotumika katika uendeshaji wa Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.NAIBU WAZIRI WA AFYA NCHINI MALAWI AFANYA ZIARA JKCI KUJIFUNZA UTOAJI HUDUMA ZA MATIBABU YA MOYO NCHINI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 6:05 PMNa: Genofeva Matemu – JKCI
18/08/2022 Naibu Waziri wa Afya wa nchini Malawi ametembelea
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya
moyo zinazotolewa pamoja na kujifunza mifumo ya Tehama inayotumika katika uendeshaji
wa huduma za matibabu katika Taasisi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam
kwa niaba ya Waziri wa Afya Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel
alisema kuwa ugeni wa naibu waziri wa afya kutoka nchini Malawi umelenga kupata
uelewa wa huduma zinazotolewa na JKCI pamoja na kujifunza mifumo ya Tehama
ambayo Tanzania inaitumia kwenye sekta ya afya ili nao waende kuboresha mifumo
ya afya nchini mwao.
Mhe. Mollel alisema kuwa uwekezaji mkubwa uliofanywa katika
taaluma ya afya na vifaa tiba imeleta tija kubwa kwani sasa nchi za Afrika na
nchi ambazo zinaizunguka Tanzania zimeanza kujifunza kupitia Tanzania na kuona
badala ya kuwapeleka wagonjwa wao India, Ulaya na Marekani waanze kuwaleta hapa
nchini.
“Upande wa upasuaji mdogo
wa moyo kupitia tundu dogo kwenye paja wataalamu wetu wameweza kufanya aina
tofauti tofauti za upasuaji ambapo hadi sasa asilimia 92 ya upasuaji mdogo wa
moyo unafanywa na wataalamu na asilimia nane iliyobaki inafanywa na wataalam
kutoka nje ya Tanzania ambapo tunawachukua wataalam hao kuja hapa kwetu
kwasababu vifaa tunavyo tunachotaka kutoka kwao ni ujuzi ambao utatuwezesha
kwenda hatua ya juu zaidi”,
“Upasuaji mkubwa wa kufungua kifua asilimia 85 za upasuaji
huo inafanywa na wataalam wa afya wazawa huku asilimia 15 za upasuaji huo
inafanywa na wataalam wa afya kutoka nje ya nchi ambao wamekuwa wakituachia
ujuzi kwa wataalamu wetu”, alisema Dkt. Mollel
Mhe. Dkt. Mollel alisema kuwa hivi sasa Taasisi ya Moyo
inapokea wagonjwa kutoka nchi 25 duniani ikiwemo Visiwa vya Comoro, Zambia,
Kenya, Congo, Malawi na nyinginezo hii inatokana na Uongozi wa Mhe. Rais Samia
ambaye tokea Mwanzo alisema kuwa anaifungua nchi kwa maana ya kufungua fursa ya
ujuzi, utalii wa kimatibabu na uduma za kibobezi za afya zinazopatikana hapa Tanzania.
Mhe. Dkt Mollel alisema kuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa
Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania amewekeza kwenye eneo la afya ambapo Afrika
hadi sasa zipo nchi chache ambazo zinafanya upasuaji wa moyo mbalimbali hivyo
kuzivutia nchi ningine kama Malawi kuona ni vyema leo kuja kujifunza kwetu.
“Mhe. Naibu waziri wa Afya kutoka Nchini Malawi Mhe. Enock
Phale amekuja hapa kwetu kwa ajili ya kuona huduma tunazizitoa na kujifunza
mifumo ya Tehama tunayoitumia katika sekta ya afya hii inaonyesha adhma ya Mhe.
Samia ya utalii wa kimatibabu inavyotekelezeka”,
Tukiwa wabunifu wakutosha kwa kuwatengenezea wataalamu wetu
ujuzi na kuvisimamia vizuri vifaa vyetu tukapata wagonjwa wengi kutoka nje ya
Tanzania mapato ya Taasisi zetu yataongezeka hivyo kuziwezesha Taasisi zetu
kujiendesha zenyewe na kupunguza kuitegemea serikali”, alisema Dkt. Mollel
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema kuwa ugeni wa Naibu Waziri wa Afya
wa nchini Malawi umelenga kujifundisha JKCI inachokifanya na itawasaidiaje kama
nchi na wao kuweza kufika Tanzania ilipo katika Sekta ya Afya.
“Malawi wanapita njia ambayo sisi tumepita huko nyuma ambapo
wagonjwa wote wa moyo, figo, saratani, mifupa na magonjwa ya damu tulikua tunawapeleka
India, Afrika ya Kusini, Ulaya na Marekani lakini baada ya uwekezaji huu mkubwa
uliofanywa na Serikali JKCI imepunguza kupeleka wagonjwa wa moyo nje ya nchi
kwa asilimia 95”,
“Katika hii miezi mitatu tumeshapata ugeni kutoka Afrika ya
Mashariki, ugeni kutoka Zambia, na tukapata ugeni kutoka Mozambique, hii ni
nchi ya nne sasa inakuja JKCI kwa ajili ya kuona nini tunafanya ili na wao
wakafanye kama sisi”, alisema Prof. Janabi
Aidha Prof. Janabi alisema kuwa Serikali ina nia kubwa katika
utalii tiba hivyo katika lile lengo la kufikisha watalii milioni 5 sekta ya
afya chini ya usimamizi wa Wizara imekusudia afya ichangie katika kuleta
watalii kupitia huduma bora na bobezi za matibabu yanayotolewa hapa nchini
yakiwemo matibabu ya moyo.
“Tunaishukuru Serikali kwa ushirikiano waliotupatia kwa
kuwekeza wataalamu na vifaa tiba vya kisasa katika Taasisi yetu, sisi kama
wataalam kazi yetu ni moja tu ya kuwahudumia wananchi wa Tanzania na nchi za
jirani za SADC ikiwemo kutangaza utalii kupitia afya”, alisema Prof. Janabi
Naye Naibu waziri wa afya Nchini Malawi Mhe. Enock Phale alisema
kuwa amekuja Tanzania kwa ajili ya kujifunza Tanzania imewezaje kufanikiwa
katika kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo na kuangalia namna ambavyo
nchi yake itaweza kuwaleta wagonjwa wa moyo badala ya kuwapeleka nchi za India
na Ulaya.
“Natamani na sisi Malawi tuwe kituo cha ubora katika kutoa huduma
za matibabu ya moyo kwani sasa tunatumia fedha nyingi kuwapeleka wagonjwa wetu
nchini India kwa ajili ya matibabu ya moyo wakati majirani zetu hapa
mmefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kutoa huduma za matibabu ya moyo”,
“Naamini kwa kuwaleta wagonjwa hapa Tanzania kutapunguza
gharama za matibabu, Malawi ni nchi wanachama wa SADC hivyo kupitia mwavuli huo
tunaenda kufanikiwa kwa wagonjwa wetu kuja kutibiwa hapa JKCI”, alisema Mhe.
Phale



0 comments: