RAISI MWINYI AAFUNGUA MKUTANO WA JUKWAA LA MAJAJI WAKUU WA NCHI ZA KUSINI NA MASHARIKI MWA AFRIKA (SEACJF. )

 
  Leo, tarehe 05 Oktoba 2026, Rais Mwinyi afungua Mkutano wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF), uliofanyika Verde Hotel, Zanzibar.

Amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimahakama wa kikanda katika kuimarisha mifumo ya utoaji haki, kubadilishana uzoefu na kuhakikisha Mahakama zinaendana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na mahitaji ya wananchi.

Ameelezea pia kuwa Mahakama zinapaswa kukumbatia ubunifu na teknolojia katika kuboresha huduma za haki, huku zikilinda misingi ya haki, usawa na taratibu stahiki za kisheria.


Aidha, amehimiza umuhimu wa kuwa na uhuru wa kifedha wa Mahakama, kwa kuhakikisha zinapata rasilimali za kutosha na zinazotabirika ili ziweze kutekeleza kwa ufanisi majukumu yao ya kikatiba.


Katika hafla hiyo, amezindua nyaraka tatu muhimu za Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (SEACJF).


Mkutano huu umewakutanisha Majaji Wakuu na viongozi wa Mahakama kutoka nchi 15 za Afrika kujadili ubunifu, ufanisi na mageuzi katika usimamizi wa Mahakama na utoaji wa haki.


Ninaamini kupitia ushirikiano huu, tutazidi kuimarisha mifumo yetu ya haki na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, kwa wakati na kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa.

















0 comments: