RAIS DK. MAGUFULI AMTEUA SIMON SIRRO KUWA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI NCHINI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:10 PM
Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Dk. John Magufuli Mei 28, 2017 amteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Habari, Ikulu jijini Dar es Salaam, Gerson Msigwa imesema, Sirro anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu ambaye kwa mujibu wa taarifa hii atapangiwa kazi nyingine.
Katika taarifa hiyo ambayo Kururugenzi ya Mawasilino ya Rais Ikulu, ameipokea kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa IGP Simon Sirro ataapishwa Mei 29, 2017 saa 3:30 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: