WATENDAJI WA CCM, UNGUJA NA PEMBA WATUNUKIWA VYETI VYA KUHITIMU MAFUNZO
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 6:29 AM
Na Is-haka Omar, Zanzibar.
NAIBU
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema Chama kitaendelea na
utamaduni wa kutoa mafunzo kwa watumishi na watendaji wake ili waweze
kufanya kazi kwa mujibu wa matakwa ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama ya
mwaka 2015/2020.
Vuai
alisema hayo leo katika hafla ya kuwakabidhi vyeti watendaji wa Chama
Cha Mapinduzi, Unguja na Pemba katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi
wa Sekretarieti katika Ofisi ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Kiswandui mjini Zanzibar.
Alisema
anamamini elimu waliyoipata matendaji hao itaweza kuwasaidia kuongeza
uwezo na ufanisi katika shughuli zao za kiutendaji katika ofisi zao kwa
wageni wanaofika katika maofisi yao.
Vuai
alieleza mafunzo hayo yametokana na matakwa ya ibara ya 188 ya Ilani
ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 inayoelekeza kutolewa kwa mafunzo
zaidi kwa makada na viongozi mbali mbali ili wawe na weledi mkubwa
katika masuala tofauti ya Chama.
Alisema
licha ya ilani ya ccm kuagiza kufufua vyuo vya uongozi na siasa vya CCM
ambavyo ni ilemi na Tunguu huku wakifikiria maamuzi ya kuendesha
mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji hao kadri uwezo wa uendeshaji wa
mafunzo utakavyoruhusu.
“
Tumieni mafunzo haya kama fursa ya kujiongeza kiutendaji ili muweze
kufanya kazi zenu kwa weledi na kujiamini zaidi.”, alisema Vuai.
Hata
hivyo aliahidi kuwa mafunzo hayo yatafanyika kwa awamu mbali mbali
kadri uwezo wa uendeshaji wake utakavyoruhusu ili Watumishi na watendaji
waweze kupata fursa hiyo ya kitaaluma.
Alifafanua
kuwa taaluma waliyopata itawasaidia katika majukumu mbali mbali
yakiwemo uchaguzi katika chama na kuwataka ifikapo mwakani watoe fomu ya
uongozi kwa kila mwanachama aliyekuwa na sifa na bila ya upendeleo ili
zoezi hilo likfanikiwe kwa asilimia kubwa.
Nae
mshiriki wa mafunzo mafunzo hayo katibu wa CCM wilaya ya Mkoani Pemba
Abdalla Yussuf Ali alisema mafunzo hayo watafanyia kazi kama
ilivyokusudiwa sambamba na kuitumia elimu waliyoipata.
Aidha alisema kuwa wataitumia elimu hiyo kwa kwa kuleta tija ya kuonekanwa kuwa ofisi zao zitakuwa ni za mfano na za kuigwa.
Mafunzo
hayo ya mwezi mmoja ziliwasilishwa mada sita ambazo ni Uanzishwaji
masjala na utunzaji kumbukumbu za Ofisi kwa usalama, Uendeshaji wa
shughuli za Ofisi na mawasiliano ya kiofisi na Taratibu za uendeshaji wa
mikutano.
Zingine
ni Dhana ya utawala bora na uzalendo katika utandawazi pamoja na
Huduma kwa mteja na utunzaji wa muda, yalikuwa na washiriki 42 kutoka
Pemba na Unguja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments: