UKINYIMWA UNYUMBA NDANI YA NDOA NENDA KASHITAKI DAWATI LA JINSIA POLISI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:24 PM
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix
Lyaniva (katikati), ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia wakati
akizindua maonyesho ya dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Temeke
viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia Mkuu wa
Polisi wa Kituo cha Chang'ombe (OCD) Msuya, Mwakilishi wa Umoja wa
Mataifa (UN), Lucy Tesha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi (SACP), Gilles Muroto na Kamishna Msaidizi wa
Polisi, Vedastus Chambu kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya
Jeshi la Polisi Nchini.
Mkuu wa Wilaya ya
Temeke, Felix Lyaniva (Wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa maonesho wa maonyesho ya dawati la jinsia na watoto Wilaya
ya Temeke katika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi.
Kutoka kulia Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Chang'ombe (OCD) Msuya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Vedastus Chambu kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Gilles Muroto na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Lucy Tesha.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Lucy Tesha akihutubia kwenye uzinduzi huo.
viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wadau na wananchi wakifuatilia hutuba za mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva.
Maofisa Wanawake wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia wakiwa kwenye Maonyesho hayo.
Wananchi na wadau wengine wakifuatilia hutuba ya mgeni rasmi
Wananchi na wadau wengine wakiwa kwenye maonyesho hayo.
Hapa ni kazi tu.
Mrakibu wa Jeshi la Polisi, (SP),
Faidha Suleiman (kushoto), ambaye anashughulikia dawati la jinsia Makao
Makuu ya jeshi hilo akimkabidhi Mgeni rasmi DC wa Temeke machapisho
mbalimbali ya ukatili wa kijinsia ikiwemo miongozo ya uanzishaji wa
dawati la jinsia na watoto ndani ya jeshi hilo.
Mrakibu
wa Jeshi la Polisi, (SP), Faidha Suleiman (kushoto), akimuelekeza Mkuu
wa Wilaya ya Temeke kuhusu kazi kubwa inayofanywa na jeshi hilo kwenye
idara ya dawati la jinsia.
Wananchi wakipata machapisho mbalimbali.
Na Dotto Mwaibale
WANANDOA wanaojimwa ujumba na wenza wao
wametakiwa kwenda kushitaki dawati la jinsia yaliyopo vituo mbalimbali
vya polisi ili kupatiwa utatuzi wa changamoto hiyo.
Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya
Temeke Felix Lyaniva wakati akizindua maonyesho ya dawati la jinsia na
watoto katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo ambayo
yalishirikisha wadau mbalimbali kutoka Hospitali ya Amana wilayani Ilala
na wananchi.
"Ukatili wa kijinsia si kupigana na
kutukana hata mume na mke wakinyimana unyumba pia ni ukatili wa kijinsia
hivyo anayejimwa hasione aibu aende kushitaki dawati la jinsia katika
kituo chochote cha polisi" alisema Lyaniva.
Lyaniva aliwataka wananchi wanao fanyiwa
vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenda kwenye dawati hilo kupata
ushauri kutoka kwa maofisa wa polisi waliopatiwa mafunzo ya kutatua
changamoto hiyo.
Katika hatua nyingine Lyaniva aliwaagiza
maofisa wa polisi wa dawati hilo kutotoa nje siri za watu wanaopeleka
malalamiko yao katika dawati hilo kwa kufanya hivyo ni kukiuka utaratibu
wa kazi.
Aliwaasa wanandoa kuwa na mshikamano na
upendo ili kuwa na familia bora na yenye maadili jambo litakalosaidia
kutokuwepo kwa watoto waliokosa maadili na kujiingiza kwenye makundi ya
kiovu kama panya road.
Lyaniva aliwaomba wanawake pale
wanapopata mafanikio ya maisha kupata fedha au kupanda vyeo kuacha
kuwadharau waume zao ili kuepusha kuvinjika kwa ndoa zao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Gilles Muroto amewataka
wananchi wasiogope kwenda kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia katika
vituo vya polisi kwani malalamiko yao yatasikilizwa kwa faragha na
maofisa maalumu wa jeshi hilo.
Maonyesho hayo yamedhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: