Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mama
Fatma Karume mara baada ya kumaliza kuhutubia katika uwanja wa Uhuru.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe
Magufuli akiagana na wananchi katika uwanja wa Uhuru mara baada ya
kumalizika kwa sherehe hizo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembea
pamoja na Askari Polisi ambao huongoza misafara ya viongozi VIP riders
mara baada ya kuwasili Ikulu wakati wakitokea katika uwanja wa Uhuru
jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe
Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan
Mwinyi mara baada ya Kuwasili katika uwanja wa Uhuru.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe
Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara
baada ya kuwasili.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu,Sera,BungeKazi,Ajira,Vijana
na Wenyeulemavu Jenister Muhagama mara alipowasili katika uwanja wa
Uhuru Jijini Dar es Salaam kushiriki nkatika sherehe za Miaka 55 ya
Uhuru wa Tanzania bara
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia) akisalimiana na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Mohamed Chande Othman alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini
Dar es Salaam kushiriki nkatika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania
bara
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa
na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika sherehe za Miaka 55
ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika leo
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuli akiwasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam
kuhudhuria katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara
zilizofanyika jana
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuli akikagua gwaride maalum la Vikosi vya Ulinzi na Usalama mara
alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kuhudhuria
katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika jana
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuli akikagua gwaride maalum la Vikosi vya Ulinzi na Usalama mara
alipowasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kuhudhuria
katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara zilizofanyika jana
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuli (katikati) akitembea kikakamavu na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange baada ya kukagua gwaride maalum la
Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika sherehe za Miaka 55 ya Uhuru wa
Tanzania bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es
Salaam. PICHA NA IKULU.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe
Magufuli leo Ijumaa ya tarehe 09 Desemba, 2016 amewaongoza viongozi
mbalimbali na wananchi kwa ujumla katika maadhimisho ya miaka 55 ya
Uhuru wa Tanzania Bara .
Maadhimisho
hayo ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara yamefanyika katika uwanja wa
Uhuru Jijini Dar es salaam na kupambwa na gwaride maalum lililoandaliwa
kwa pamoja na Majeshi ya Ulinzi na Usalama ikiwa ni pamoja na Jeshi la
wananchi wa Tanzania JWTZ,Jeshi la Polisi,Jeshi la Magereza na Jeshi la
Kujenga Taifa.
Akizungumza
na halaiki ya watanzania waliohudhuria sherehe hizo Rais Dkt Magufuli
amesema mwaka jana alilazimika kuzuia kufanyika kwa shamrashamra ya
maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Bara kutimiza miaka 54 kwa kuwa alikuwa
na mwezi mmoja tu tangu aingie madarakani na kuitaja sababu ya pili
kuwa ni bajeti kubwa ya shilingi bilioni nne iliyokuwa imetengwa kwa
ajili ya maadhimiso hayo na kuona ni vyema ikaelekezwa katika upanuzi wa
barabara ya Alli Hassani Mwinyi yenye urefu wa kilomita 4 ambayo
inatumiwa na Watanzania wote badala ya fedha zile kutumiwa na wachache.
"Sherehe
za miaka 55 nimeamua zifanyike kwasababu gharama zake ni ndogo
sana,kwanza hakuna hata chakula baada ya sherehe hii,hakuna dhifa ya
Taifa ,tukimaliza hapa tumemalizana ,lakini pili niliamua sherehe hii
niifanye hapa Dar es Salaam kwa kuwa yatakuwa ni maadhimisho ya mwisho
kufanyika jijini Dar es salaam na kwamba ni matumaini yake kuwa sherehe
za mwaka kesho zitafanyika makao makuu ya nchia mbayo ni Dodoma"
Ameongeza
kuwa sherehe za Uhuru ni tukio kubwa sana katika Taifa na hivyo
serikali itaendelea kuipa umuhimu siku hiyo na kuiadhimisha.
Rais Dkt
Magufuli pia amezitaja changamoto ambazo serikali ya awamu ya tano
inazokumbana nazo kuwa ni pamoja na ufisadi na rushwa ndani ya baadhi ya
watendaji na kuongeza kuwa mpaka sasa hivi wafanyakazi hewa wamefikia
elfu kumi na tisa huku kaya masikini hewa zinazonufaika na mfuko wa
TASAF zikiwa ni elfu 55 na wanafunzi hewa mpaka sasa hivi wamefikia
elfu sitini na tano.
"Serikali
ya awamu ya Tano itaendelea kuchukua hatua kali ikiwa ni pamoja na
kuwatumbua hadharani wale waliozoea kutumbua hadharani mali za
watanzania na tuataendelea kuchukua hatua kali katika masuala ya rushwa
na ufisadi,kwasababu rushwa ni saratani" Rais
Dkt Magufuli amepongeza pia jitihada zilizofanywa na watangulizi wake
katika maendeleo ya Tanzania na kuwashukuru kwa niaba ya watanzania huku
akiwataka watanzania wote bila ya kujali dini,itikadi za kisiasa na
makabila yao kuendelea kudumisha amani na mshikamano ili Tanzania iweze
kupiga hatua za kimaendeleo kwa haraka.
"Hivyo
basi tuendelee kuilinda amani yetu na kuwafichua watu wenye nia ovu ya
kuhatarisha amani yetu na sambamba na kulinda amani yetu hatuna budi
kudumisha umoja na mshikamano wetu ambao ni nguvu na silaha yetu kubwa
kama Taifa,lakini pia tuendelee kuulinda muungano wetu ambao ni silaha
kubwa ya umoja wetu ili Tanzania tuendelee kwenda mbele"
Hii ni
mara ya kwanza kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli kuhudhuria na kuhutubia
katika sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara tangu aingie madarakani.
Emmanuel BuhohelaKaimu Mwandishi wa habari Msaidizi wa Rais.Dar es Salaam
09 Desemba, 2016.
0 comments: