MADIWANI WALIA NA UHALIBIFU WA MAZINGIRA MKOANI KIGOMA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 4:53 AM
NA MAGRETH
MAGOSSO,KIGOMA
BARAZA la
Madiwani wilaya ya Kakonko mkoani kigoma wamesikitishwa na kitendo cha
uharibifu wa mazingira unaofanywa na wakimbizi waishio katika Kambi ya Mtendeli
iliyopo humo,huku ofisi za idara ya wakimbizi na stahiki za malipo
wakizielekeza wilaya ya kibondo,ambapo ni kinyume cha sheria husika.
Hayo
yalibainikamwishoni mwa wiki katika
kikao cha Baraza hilo katika kipindi cha
maswali na majibu katika kutatua kero za umma kupitia idara mbalimbali baraza hilo lilihitaji majibu sahihi kutoka
kwa mkuu wa kambi kigoma sababu ya kuweka ofisi kibondo na kulipa stahiki wakati
uharibifu wa mazingira unafanywa wilaya ya kakonko.
Awali
Diwani Steven Mnigankoko alisema changamoto ya ukataji miti holela umekithiri
wilayani humo,huku stahiki za kuhifadhi wakimbizi zikielekezwa wilaya ya
kibondo hali kadhalika ofisi za idara hiyo ipo huko ilihali janga la ukataji
miti unafanyika kakonko na kwa mujibu wa sheria stahiki na ofisi ziwepo eneo linalohifadhi
wakimbizi na si vinginevyo.
Akiongezea
hilo Mbunge wa Jimbo la Buyungu Kasuku Bilago alisema kisheria walihitajika
kuweka ofisi na stahiki katika eneo linalohifadhi wakimbizi kwa kutoa huduma za
kijamii katika maeneo yanayoathirika na uwepo wao ambapo miti mingi inatumika
hovyo hali inayotishia mabadiliko ya tabia nchi,kwa kuwa hakuna jitihada za
makusudi kupunguza uharibifu huo.
Akijibia
hilo Mkuu wa Kambi ya wakimbizi Mtendeli Innocent Mwaka alisema changamoto hiyo
inatokana na historia ya wilaya ya kibondo ambayo ilibeba kambi zaidi ya mbili
na kugawanywa kwa wilaya hizo ni chachu ya ofisi kubaki humo na stahiki kwa
ujumla.
Akiongezea
hoja hiyo Mwenyekiti wa halmashauri ya kakonko Juma
Maganga alisema changamoto hiyo inajulikana na waziri mwenye dhamana na
linafanyiwa kazi na katibu wa wizara ya mambo ya ndani hivyo hawana budi
kuliacha kama lilivyo hadi hapo taratibu za serikali kuu itakapotoa tamko
rasmi.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: