KAYA 307 ZAGUNDULIKA HAZINA VIGEZO MRADI WA TASAF BUHIGWE MKOANI KIGOMA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 8:57 AM
NA MAGRETH
MAGOSSO,KIGOMA
Mkuu wa wilaya
ya
Buhigwe Mkoa wa Kigoma Kanal Marko Gaguti amethibitisha kuwepo kwa kaya
307 katika wilaya hiyo, zilidanganya tarifa zao hatimaye kunufaika na
mradi wa Mfuko wa kusaidia kaya maskini
sana, TASAF wakati hazina sifa na vigezo wa kunufaika na mfuko huo.
Akitoa kauli hiyo
katika ziara ya siku 10 ya kukagua kaya zilizokuwa katika mpango wa kupunguza
umaskini kwa walengwa wa TASAF Gaguti alisema kwa Tasaf awamu ya tatu wasio na
sifa wataondolewa kwa kuwa hawana vigezo hali iliyochangia wananchi wengi
waliongia kwa hila kukimbia kaya zao na katika hili wamejiondoa wenyewe.
“ziara hii ya
nyumba kwa nyumba inashirikisha viongozi kuanzia ngazi ya kijiji, kata na wilaya
ili kubaini uhalisia wa maisha ya sifa ya walengwa wa mfuko wa TASAF , kubaini
maisha yao na waliodanganya wataondolewa na kuingizwa wenye sifa, serikali ina
dhati ya kupunguza umaskini, viongozi shirikianeni na serikali yenu” alifafanua
Kanal Gaguti.
Kwa upande wa
Mratibu wa TASAF wilaya ya Buhigwe, Chubwa Deogratius alisema katika ziara ya
juzi walibaini kaya mbili katika kata ya Mnanila hazina vigezo vya kupata fedha katika mfuko huo ambao
ni Anjelina Josia na Veronika James hawana sifa na vigezo vya kutumia fursa
hiyo na wanaendelea kupita nyumba hadi nyumba kwa wanufaika wote wa awamu ya
tatu ili kujiridhisha na tarifa za awali zilizowaingiza katika mpango huo.
Akisisitiza hilo
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu, Emanuel Maganga alisema kwa
yeyote aliyewahi kuingizwa katika mpango wa TASAF na hana vigezo na sifa za
kuwa miongoni mwa wanufaika watafikishwa katika vyombo vya sheria na watalipa
fedha zote walizowahi kulipwa na mfuko huo, kwa kuwa ndio chanzo cha kikwazo cha
maendeleo kwa walengwa wa mfuko huo.
Maganga aliongeza
kuwa, wananchi waliopokwa haki za kuingizwa katika mfuko huo wasubiri mwakani
pindi utakapoisha ukomo wao na walengwa wataingizwa ili wahujumu wa hilo
watapatiwa haki zao kwa mujibu wa sheria za nchi na kuomba wawe wavumilivu
zaidi ili kuwapa fundisho wananchi wenye tabia ya uongo na ktumia rushwa ili
wapate haki za wenzao.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: