JESHI LA SYRIA LAENDELEZA MASHAMBULIZI DHIDI YA MAGAIDI HUKO HALAB
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:05 AM
Duru za Syria zimearifu kuwa jeshi la nchi
hiyo limeendelea kuwashambulia magaidi ili kuukomboa kikamilifu mji wa
kihistoria wa Halab yaani Aleppo.
Duru za kijeshi za Syria zimeripoti kuwa wanajeshi wa nchi hiyo
leo wamefanya mashambulizi ya nchi kavu na anga na kuendelea kusonga
mbele huko mashariki mwa mji wa Halab ili kuwafurusha kikamilifu magaidi
katika mji huo. Kituo cha Usuluhishi cha Russia kimeripoti kuwa raia
zaidi ya elfu kumi wakiwemo watoto elfu nne wameondoka katika maeneo
yanayoshikiliwa na magaidi huko Aleppo katika muda wa saa 24
zilizopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: