NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
KUTOKANA na kupanda kwa ushuru wa
bidhaa ya mkaa ,chama cha wauza mkaa mkoani kigoma wameadhimia kuuza gunia moja
lenye ujazo wa kilo 50 kwa kiasi cha sh.50,000 ifikapo Desemba mosi mwaka huu.
Akifafanua hilo mbele ya gazeti
hili Mwenyekiti wa chama hicho Fadhili Kiswaga alisema serikali ya awamu ya
tano si serikali ya kufanya biashara kwa ujanjaujanja badala yake wadau wa mali
asili hasa misitu hawana budi kufanya biashara kwa mujibu wa sheria na taratibu
za wizara husika.
Kiswaga alisema, kupanda kwa
gharama hiyo inachangiwa na gharama za ushuru wa serikali kuu ambapo hutozwa
fedha sh.240 kwa kilo moja,serikali ya wilaya ambayo wanalangua mkaa wanatozwa
sh.16,600 kwa kila gunia,kibali cha usafirishaji (TP)sh,7,500 sanjari na Sh.1,000 kwa ajili ya upandaji miti.
“tunalangua kwa wakulima gunia
moja kwa sh.12,000 ,jumla ya gharama ni sh.47,100 hali inayotulazimu kuuza kwa jumla
kwa bei hiyo kwa walaji wa nyumbani na kwa wateja wanaouz mitaani watalangua
kwa sh.55,000 ili kila mtu achangie pato la taifa na si kukwepa sheria ambayo
inanufaisha wachache” alibainisha Kiswaga.
Alisema awali walikuwa wakiuza
gunia moja kwa sh.25,000 lakini katika usafirishaji wa zao hilo kuna shubiri na
tamu ili kufikisha bidhaa kwa walaji,hali iliyopeleka chama kujipanga na
kuratavyowakabili ili kufanya biashara kwa uwazi ili kuziba mianya ya rushwa
,huku akikiri serikali ya sasa ni sheria
bila shuruti.
Aliomba serikali isaidie
kupunguza gharama za zao hilo kwa kuweka risiti katika vituo vya maliasili
vilivyopo katika eneo la mizani simbo
ili kuepuka urasimu wa kupata risiti za ulipiaji wa zao hilo,ambapo kwa sasa
wanalazimika kwenda halmashauri ya lugufu kulipia ilihali kuna uwezekano wa
kuondoa usumbufu huo.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: