CHADEMA YAWANOA VIONGO WAKE WA MABARAZA WILAYA YA NYAMAGANA MKOANI MWANZA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 11:00 AM
Katibu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Micus
(kulia), akizungumza juzi kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya
Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Lengo lilikuwa ni
kuimarisha mabaraza hayo kwa ajili ya utendaji kazi wake ikiwemo
kuhakikisha wanachama wapya wanaendelea kujiunga na chama chadema ili
kukifanya kuendelea kuwa chama cha upinzani chenye nguvu nchini.
Chama hicho kililaani zoezi la
kuwahamisha machinga kutoka katikati ya Jiji la Mwanza huku mazingira
rafiki yakiwa bado hayajaandaliwa ambapo Micus alisema hatua hiyo
inaweza kusababisha vijana na akina mama wengi kukosa mwelekeo wa
kujitafutia kipato kwa njia sahihi ambapo walihimiza machinga hao
kutengenezewa mazingira bora ya kufanyia biashara zao.
Na BMG Habari
Baadhi ya viongozi wa mabaraza ya
Chadema wilayani Nyamagana wakimsikiliza Katibu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Micus (kulia), wakati
akizungumza kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya
Nyamagana mkoani Mwanza.
Diwani wa Kaya ya
Butimba, John Pambalu, akizungumza juzi kwenye semina kwa viongozi wa
Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Baadhi ya viongozi wa mabaraza ya
Chadema wilayani Nyamagana wakimsikiliza diwani wa Kata ya Butimba, John
Pambalu, wakati akizungumza kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya
Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Baadhi ya viongozi wa mabaraza ya
Chadema wilayani Nyamagana, wakifuatilia kwa makini semina iliyotolewa
kwa ajili ya kuimarisha uhai katika utendaji wao wa kazi ili
kujiimarisha zaidi.
Viongozi mbalimbali Chadema Wilayani Nyamagana
Katibu wa Chadema Kanda ya Ziwa, Mechack
Micus, akizungumza nje ya semina kwa viongozi wa mabaraza ya Chadema
Wilayani Nyamagana.
John Amos, Mwenezi BAVICHA Kata ya Igoma
Jijini Mwanza, akizungumza nje ya semina ambapo alipongeza semina hiyo
kwamba itaendelea kukiimarisha chama.
Seko Jabanhya ambaye ni Mwenezi wa
Vijana Chadema Wilaya ya Nyamagana, akizungumza baada ya semina kwa
viongozi wa mabaraza Chadema wilayani Nyamagana. Alisema itasaidia chama
kujiimarisha zaidi na kuendelea kuwatetea vyema wananchi.
Eather Alphaxard ambaye ni mwakilishi
kutoka Kata ya Igoma ndani ya BAVICHA wilaya ya Nyamagana alisema semina
hiyo itasaidia kuimarisha misingi ya viongozi wa mabaraza ndani ya
chama.
Katikati ni Wilbert Mandago ambaye ni
Afisa Bunge na Halmashauri Chadema akiteta jambo na viongozi wengine wa
Mabaraza Chadema wilayani Nyamagana
Picha ya pamoja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: