Wafanyaziara (mazuwwar) zaidi ya 80 wamekufa
shahidi leo kufuatia shambulio la kigaidi la bomu la kutegwa garini
lililowalenga katika mji wa Hillah kusini mwa Iraq.
Taarifa za awali zinasema kuwa,
wengi wa waliouawa shahidi katika shambulio hilo la kigaidi ni
wafanyaziara wa Kiirani. Vyombo vya usalama vya Iraq vimetangaza kuwa,
mlipuko huo wa bomu la kutegwa garini ulitokea katika kituo kimoja cha
kujazia mafuta (petrol station) katika mji wa Hilla na kwamba, Mazuwwar
hao waliokwenda nchini Iraq kwa ajili ya ziara ya Imam Hussein as
walikuwa njiani kurejea makwao.
Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran sambamba na kulaani shambulio hilo la kigaidi
ametangaza kuungana pamoja na familia za Wairanmi waliopoteza ndugu zao
katika shambulio hilo la kigaidi. Amesema, jinai hiyo ni radiamali ya
kushindwa mfululizo magaidi hao huko Iraq.
Bahram Qassemi amebainisha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya iran itaendelea kuwa kando ya taifa la Iraq katika kupambana na ugaidi.
No comments:
Post a Comment