MUUNGANO UNAO NGOZWA NA SAUDIA WATANGAZA USITISHAJI WA MAPIGANO YEMEN
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:21 PM
Muungano
unaongozwa na Saudi Arabia Jumamosi (19.11.2016) umetangaza usitishaji
wa mapigano wa masaa 48 kwa masharti waasi wa Kishia wauzingatie na
kuruhusu kufikishwa kwa misaada ya kibinadamu katika miji iliozingirwa.
Hata
hivyo dakika chache baada ya kuanza utekelezaji wake wanaharakati katika
mji wa Taiz wamesema kwamba mashambulizi ya mizinga ya waasi
yanaendelea katika mji huo wakati msemaji wa kijeshi anayehusiana na
waasi amesema kwamba hakuna mapigano yaliyositishwa.
Kanali
Sharaf Loqman msemaji huyo wa kijeshi ameliambia shirika la habari la AP
kwamba hakuna mapigano yaliyositishwa katika medani yoyote ya
mapambano. Amesema waasi wanaunga mkono usitishaji kamili wa uhasama
lakini kiuhalisia kwa sasa pande zote ziko katika mapigano.
Shirika
la habari la Saudia SPA limekuwa na taarifa kutoka kwa muungano
unaogozwa na Saudi Arabia inayosema usitishaji wa mapigano utaanza
kutekelezwa sasa sita mchana saa za Yemen hapo Jumamosi na kwamba
usitishaji huo unaweza kuongezewa muda.Muungano huo umewaonya waasi
wanaojulikana kama Wahouthi dhidi ya kujihusisha kijeshi kwa njia yoyote
ile.
Usitishaji
huo wa mapigano unakuja wakati vikosi vilivyo tiifu kwa serikali
inayotambuliwa kimataifa inayoungwa mkono na Saudi Arabia vikisonga
mbele huko Taiz mji ambao umezingirwa na waasi kwa mwaka mmoja sasa.
Dai la muungano
Muungano
huo ulikuwa ukidai Wahouthi watume wawakilishi wao kukutana na kamati ya
kusitisha mapigano ilioko katika mji wa kusini wa Saudi Arabia ili
kuandaa mipangilio ya usalama na kijeshi kukomesha udhibiti wa waasi kwa
miji kadhaa ilioko kaskazini mwa Yemen ukiwemo mji mkuu wa Sanaa.
Wakati
muungano huo ukisisitiza kwamba usitishaji huo wa mapigano unakusudia
kufunguwa njia ya amani haukufafanuwa iwapo inaukubali mpango wa amani
wa Umoja wa Mataifa ambao unamweka kando Rais Abed Rabbo Mansour Hadi na
kuwapa nafasi waasi kushirikiana madaraka.
Usitishaji
huu wa mapigano pia unakuja siku mbili baada ya mpango wa awali wa
kusitisha mapigano chini ya usimamizi wa Marekani kwenda kombo.Waziri wa
mambo ya nje wa Marekani John Kerry ambaye amekutana na wawaklishi wa
Wahouthi nchini Oman wiki hii ameweka tarehe 17 Novemba kuwa ni siku ya
kuanza kwa usitishaji wa mapigano.
Mpango
huo ulikataliwa mara moja na serikali ya Hadi ambayo inamshutumu Kerry
kwa kufanya makubaliano ya upande mmoja.Muungano huo unaongozwa na Saudi
Arabia haukutowa kauli yoyote ile kuhusu tangazo hilo la Kerry.
Maafa na madhara
Mzozo
nchini Yemen umeigawa nchi hiyo katika maeneo yanayohasimiana ambako
huko kaskazini yakikaliwa na Washia na huko kusini yakikaliwa na Wasuni
chini ya udhibiti wa muungano na Saudi Arabia.
Muungano
huo uliigilia nchini Yemen hapo mwezi wa Machi mwaka 2015 kufuatia ombi
la Hadi ambaye alilazimika kuikimbia nchi hiyo wakati Wahouthi
walipojiunga na vikosi tiifu kwa Rasi Ali Abdullah Saleh aliyeondolewa
madarakani kwa kutoka kwenye eneo lao kaskazini mwa nchi hiyo na kuuteka
mji mkuu na kuanza kusonga mbele kulekea kusini mwa nchi hiyo.
Mashambulizi
ya anga ya majeshi ya muungano na mapigano yanayoendelea yamesababisha
vifo vya raia 4,000 na kujeruhi wengine maelfu.Mzozo huo umewapotezea
maakazi watu milioni tatu na kuliweka taifa hilo la kimaskini katika
ulimwengu wa Kiarabu kwenye ukingo wa baa la njaa.DW
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: