DC- KANALI NDAGALA AGIZA JESHI LA POLISI KUWAONDOA WALIOJENGA ZIZI LA MIFUGO KATIKA KITUO CHA AFYA- KAKONKO

MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala ameliagiza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Serikali ya Kata ya Gwanumpu kuwaondoa mara moja wafugaji waliovamia na kujenga zizi la Ng’ombe karibu na chanzo cha maji na huduma za kijamii ilihali wanajua ni kunyume cha taratibu na sheria husika


Akithibitisha kauli hiyo juzi wilaya ya Kakonko alipotembelea baadhi ya vijiji vya wilaya hiyo ambapo awali alipata malalamiko kutoka kwa wananchi  kuwa kuna changamoto ya kuingiliana  maeneo ya mashamba na baadhi ya wafugaji kukiuka sheria za mamlaka kwa kujenga zizi la mifugo katika kituo cha afya,shule na chanzo cha maji ni kero kwa serikali, hali inayoashiria kutokea matukio ya mauwaji huku akizitaka mamlaka husika kuweka matumiza bora ya adhi sanjari na wananchi wafuate taratibu na sheria  zilizowekwa.

‘’kero hii huanza taratibu yapoachwa uongezeka  mwishowe kusababisha madhara makubwa na kupelekea watu kuuwana kisa mgogoro wa ardhi kwa ajili ya malisho na kilimo hivyo ,isipodhibitiwa  vifo na upotevu wa  rasilimali nuvu kazi ya Taifa ‘’alisema Kanali Ndagala

James Myelekano,  ni mmoja wakazi wa Kijiji cha Bukiliro, Kata ya Gwanumpu chenye wafugaji wengi  alisema kuwa  viongozi wa vijiji watenge maeneo yanayoeleweka  kwa jamii hizo,na sheria,taratibu ziwe wazi ,ili kuepusha majanga, nakuiomba  serikali iwaondoe  haraka waliovamia maeneo ya mashamba kwa ajili ya mifugo .

Kwa niaba ya wakulima  Deogratias Kavano alifafanua kuwa, kuna mfugaji mmoja amehamishia mifugo yake katika eneo la vyanzo vya maji na kuchunga mifugo yake katika sehemu zinazotolewa huduma za afya na shule na kukataa kutoa mifugo yake .

Akithibitisha hilo Mwenyekiti wa kijiji cha Gwanumpu Festo Sulila  akiri   Mfugaji huyo  kujenga Zizi la Ng’ombe jirani na Kituo cha Afya  cha Gwanumpu na Shule ya sekondari  ya Gwanumpu  licha ya kutostaili kuwepo kwa zizi hilo katika eneo hilo la makazi ambapo inawapa kero ya harufu mbaya lakini anakataa kutoka hapo.
Mwisho.

0 comments: