WAFANYAKAZI MUHIMBILI WAONGEZA MAPATO HADI KUFIKIA SH 4.8 BILIONI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 5:52 AM
Kaimu
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence
Museru akizungumza katika hafla ya kuwatunukia vyeti wafanyakazi bora
54. Hafla hiyo imefanyika katika hospitali hiyo.
Na John Stephen, MNH .
Dar es
Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanikiwa kuongeza mapato
kutoka Sh 2.3 bilioni yaliyokuwa yakikusanywa Desemba mwaka jana hadi
kufikia Sh 4.8 bilioni Mei mwaka huu. Hayo
yamesemwa LEO na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence
Museru wakati hafla ya kutunuku vyeti kwa wafanyakazi bora wa hospitali
hiyo.
Hospitali
hiyo imefanikiwa kuongeza mapato kutokana na juhudi za wafanyakazi
ambao wanafanya kazi kwa ari kubwa ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa. Pia,
wafanyakazi wamehamasika kutokana na mkurugenzi huyo kuwajali
wafanyakazi na kusikiliza kero na kuzitatua kwa wakati kwa mfano hivi
karibuni alilipa malimbikizo ya wafanyakazi. Profesa Museru amesema
mapato hayo yameongezeka kutokana na juhudi za wafanyakazi ambao
wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii na hivyo kusababisha mapato hayo
kufikia Sh 4.8 bilioni.
“Mafanikio
haya yametokana na juhudi za wafanyakazi. Mwaka jana niliwaomba
wafanyakazi wafanye kazi kwa bidii, na wao walikubali. Imani yangu ni
kwamba posho kwa wafanyakazi wangu zitaanza kulipwa baada ya bodi
kupitisha ombi la kuwaongezea. Nafikiri tukiwaeleza vizuri bodi
watatuelewa na hivyo wafanyakazi watapata kile tulichowaahidi,” amesema
Profesa Museru.
Mkurugenzi
huyo amesema kwamba hospitali imepata mafanikio makubwa yakiwamo
kuongeza huduma za afya kwa mfano kuanzishwa kwa huduma ya kusafisha
figo, kuongeza wodi kwa wagonjwa wanaohitaji uangali maalumu, huduma za
matumbo na kuboreshwa kwa mazingira ya kutolea huduma.
Amesema
hospitali hiyo inajitahidi kuongeza mapato zaidi ili iweze kulipia
huduma za umeme, huduma za simu, ankra za maji pamoja na kudi za
majengo.
“Sisi
hatufanyi biashara bali tunatoa huduma kwa wagonjwa, tunapaswa kuongeza
mapato ili kulipia huduma kutoka kwa washirika wetu akiwamo Tanesco,
kulipia maji na huduma za simu,” amesema Kaimu Mkurugenzi huyo.
Akizungumzia
changamoto, Profesa Museru amesema sehemu zinazotumika kutoa huduma
zinatakiwa kukarabatiwa. Amesema miundombinu inapaswa kukarabatiwa kwa
kuwa imekuwa ikichakaa kutokana na kuongezeka kwa wagonjwa hospitali
hapo.
“ Majengo ya hospitali hayajakarabatiwa karibu miaka 20, hivyo tunapaswa kukarabati sasa,” amesema.
Pia Profesa Museru amewapongeza wafanyakazi bora ambao wametunukiwa vyeti baada ya kuibuka kuwa wafanyakazi bora. Wafanyakazi wa hospitali hiyo wakiwamo madaktari na wauguzi wakimsikiliza Profesa Museru Mwenyekiti
wa TUGHE Tawi la Muhimbili, Mziwanda Chimwege akisoma risala kwa mgeni
rasmi, Profesa Museru katika hafla ya kuwakabidhi vyeti wafanyakazi boraWafanyakazi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Mwenyekiti wa TUGHE, Mziwanda Chimwege.
William
Chimwege wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Hospitali hiyo, akipokea
cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Uuguzi, Agness Mtawa baada ya kuchaguliwa
kuwa mfanyakazi bora. Mkurugenzi
wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru akimkabidhi cheti mfanyakazi
wa Idara ya Ajira na Mafunzo, Farisha Jumanne baada ya kuchaguliwa kuwa
mfanyakazi bora. Wafanyakazi
wa Muhimbili wakiserebuka baada ya wafanyakazi bora kutunukiwa vyeti.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: