SIMBA APIGWA 2-0 NA JKT RUVU KATIKA FAINALI ZA FASDO FOOTBALL CUP JIJINI DAR

 Timu ya Simba chini ya Umri wa Miaka 20 wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpira kuanza dhidi ya JKT Ruvu
 Timu ya JKT Ruvu chini ya umri wa miaka 20 wakiwa katika picha ya pamoja kabla mechi haijaanza dhidi ya Simba
 Mkurugenzi mtendaji wa Faru Arts and Sport Development Organization (FASDO)  Tedvan Chande Nabora akikagua timu zote mbili kabla ya mpira haujaanza
 Mpira ukiwa unaendelea huku ikiwa ni vuta nikuvute ambapo JKT Ruvu waliibuka washindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba, pia simba walikosa penalti.
 Mgeni Rasmi katika Mashindano ya mpira wa Miguu wa FASDO, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole akiwa anafuatilia Mchezo huo
Mashabiki wa upande wa Simba wakifuatilia kwa makini Mchezo huo
 Mashabiki upande wa JKT Ruvu wakiwa wanafuatilia kwa makini mchuano huo
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole akionesha kombe pamoja na zawadi ya mshindi wa kwanza kiasi cha Tsh 2,000,000 wakati wa fainali hizo, zilizofanyika katika viwanja vya JMK jijini Dar

Refa Bora katika mashindano ya mpira wa miguu ya FASDO akikabidhiwa zawadi ya Kitita chake cha Laki moja
 Washindi wa pili katika Mchezo huo timu ya Simba wakiwa wanapokea zawadi yao ya Tsh 1,000,000
Mgeni rasmi katika fainali hizo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole akikabidhi kitita cha Tsh 2,000,000 kwa nahodha wa timu ya JKT Ruvu ambao ndio waliibuka kidedea.
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole akikabidhi Kombe kwa timu ya JKT Ruvu baada ya kuibuka washindi
 Wakiwa wanalipokea rasmi kombe lao baada ya ushindi
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Humphrey Polepole (Kulia) akikabidhiwa zawadi ya picha  kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya FASDO
 Timu ya JKT Ruvu wakifurahi baada ya kuibuka washindi.

0 comments: