Na Dotto Mwaibale
UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya
Tiba Shirikishi Muhimbili (MUHAS) umezuia mkutano uliokuwa ufanywe na
baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho na Waziri Mkuu wa zamani Edward
Lowaasa.
Mkutano huo ambao ulikuwa ufanyike na
baadhi ya vijana wa kikristo ambao ni wanafunzi wa chuo hicho ulikuwa
pangwa kufanyika juzi chuoni hapo kuanzia saa za mchana.
Akizungumza mtandao wa www. habari za jamii.com
mmoja wa wanafunzi hao ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema
maandalizi yote ya mkutano huo ambao ulikuwa baada ya ibada yalikuwa
yamekamilika.
"Tulifanya taratibu zote ikiwa ni pamoja
na kutoa taarifa kwa uongozi wa chuo ambao ulitukubalia na kumualika
ndugu Lowassa lakini tumeshangazwa na zuio lililotolewa na uongozi wa
chuo" alisema mwanafunzi huyo.
Mwanafunzi huyo alisema kuwa saa sita
mchana wakati wakimsubiri mgeni rasmi Edward Lowassa awasili mkuu wa
chuo hicho na viongozi wengine waliwaita na kuwaeleza kwamba mkutano huo
umewekewa zuio kutoka juu hivyo hautafanyika bila ya kutoa sababu .
Msemaji wa Lowassa Abubakar Lihongo
alisema wanafunzi hao baada ya kuzuiliwa kufanya mkutano huo walimuomba
radhi Lowassa na kumueleza watamualika tena kipindi kingine wakiwa
tayari.
"Mimi naona zuio hilo linatokana na
masuala ya kisiasa lakini kuna barua ya wanafunzi hao ipo katika
mitandao ya kijamii mkiipata mnaweza kupata picha halisi" alisema
Liongo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: