ZIARA YA KIHISTORIA YA DKT. MAGUFULI NCHINI RWANDA, UHUWA TANZANIA NA RWANDA WAONYESHA MWANGA MPYA

 Rais wa Rwanda Paul Kagame akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa daraja la Rusumo, hivi karibuni ambapo rais alisafiri hadi nchini Rwanda kwa ziara ya ihistoria ya siku mbili na kujenga mwanzo mpya katika uhusiano baina ya nchi hizi mbili ambao kwa kiasi fulani ulizorota mwioshoni mwa utawala wa serikali ya awamu ya nne. Akiwa nchini Fwanda, Rais alihudhuria kumbukumbu ya kila mwaka ya wahanga wa mauaji ya halaiki nchini humo ya mwaka 1994 ambapo watu wanaokadiriwa kufikia milioni moja (1,000,000), wengi wao watutsi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa. Rais  amerejea nyumbani Jumatano Aprili 7, 2016 na kulakiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi wa serikali ya mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange, kuu wa jeshi la polisi IGP, Ernest Mangu

























0 comments: