NAIBU KATIBU MKUU WA CCM, RAJAB LUHWAVI AZUNGUMZA NA MAKATIBU WA MATAWI NA KATA WILAYA YA DODOMA MJINI LEO

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akiwasalimia baadhi ya viongozi baada ya kuwasili Ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma, kuzungumza na Makatibu wa CCM wa matawi na Kata katika wilaya ya Dodoma mjini. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, Paulo Luhamo na Katikati ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Salum Kalli.
 Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Salum Kalli akizungumza maneno ya utangulizi kabla ya kuanza kikao hicho
 Makatibu wa matawi na Kata za wilaya ya Dodoma mjini, wakiwa tayari ukumbini kuzungumzana Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi katika Ukumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi (wapili kulia) akiwasili katika ukumbi wa Sekretarieti katika Ofisi ya Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma,  kuzungumza na Makatibu wa CCM wa matawi na Kata katika wilaya ya Dodoma mjini. Kulia ni Katibu wa CCM wa mkoa wa Dodoma, Jamila Yusuph.
 Katibu wa CCM wilaya ya Dodoma mjini akihamasisha, baada ya Luhwavi (katikati) kuwasili ukumbini. kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma Jamila Yusuph
 Wajumbe wakiwa ukumbini Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini Paulo Luhamo akimkaribisha Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma ili kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu kuzungumza katika kikao hicho
 Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) kuzungumza katika kikao hicho
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akizungumza na Makatibu wa CCM wa matawi na Kata katika wilaya ya Dodoma mjini, katika Ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma,  Kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Dodoma mjini, Paulo Luhamo
 Maofisa waandamizi wa Chama wakifuatilia kwa karibu kikao hicho
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akizungumza na Makatibu wa CCM wa matawi na Kata katika wilaya ya Dodoma mjini, katika Ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. 
Baadhi ya wajumbe wakitoa yao ya moyoni kuhusu kero au changamoto wanazoziona katika utumishi wa Chama. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

0 comments: